Uzayuni

Ismail Ridhwan: Jinai ya kumuua shahidi Ammar Mefleh haitasalia bila jibu

Ismail Ridhwan: Jinai ya kumuua shahidi Ammar Mefleh haitasalia bila jibu

Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameeleza kuwa, jinai ya kumuua shahidi Ammar Mefleh ni jinai ya kivita na dhidi ya binadamu na haitasalia bila jibu. Mwanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel juzi Ijumaa alikabiliwa na muqawama wakati alipojaribu kumtia nguvuni Ammar Mefleh katika kitongoji cha Huwara…

Kombe la Dunia; mwanajeshi Mzayuni akimbia haraka Qatar baada ya kugunduliwa uhakika wake

Kombe la Dunia; mwanajeshi Mzayuni akimbia haraka Qatar baada ya kugunduliwa uhakika wake

Mwanajeshi mmoja Mzayuni aliyejipenyeza nchini Qatar kwa sura bandia ya msanii wa vichekesho, amekimbia haraka nchini humo baada ya Mpalestina mmoja kumgundua na kufichua uhakika wake kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter. Tovuti ya habari ya al Khalij al Jadid imeripoti habari hiyo leo Jumapili na kuongeza kuwa, Samar Dahmash Jarrah, mwandishi Mpalestina raia wa Marekani…

Wananchi wa Argentina waandamana kuliunga mkono taifa la Palestina

Wananchi wa Argentina waandamana kuliunga mkono taifa la Palestina

Makumi ya wananchi wa Argentina wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Buenos Aires na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa taifa madhulumu la Palestina. Waandamanaji hao wakiwa wamebeba bendera za Palestina wakiwa pia na mabango na maberamu  yaliyoandikwa jumbe mbalimbali za kuwaunga mkono Wapalestina walikusanyika mbele ya ubalozi wa Israel mjini Buenos Aires…

Sheikh Ali Da’mush: Mshindi halisi wa Kombe la Dunia Qatar ni Palestina

Sheikh Ali Da’mush: Mshindi halisi wa Kombe la Dunia Qatar ni Palestina

Naibu wa Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mshindi halisi wa fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar ni taifa la Palestina kutokana na wimbi kubwa la wachezaji na mashabiki wa soka kuwaunga mkono wananchi wa Palestina. Sheikh Ali Da’mush amebainisha kuwa, matukio mbalimbali yanayoshuhudiwa hivi sasa katika mashindano…

Kimya cha jamii ya kimataifa na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina

Kimya cha jamii ya kimataifa na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina

Mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya raia wa Palestina yanaendelea katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu katika kivuli cha kimya na upuuzaji wa jamii ya kimataifa. Mashambulizi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni yameshtadi katika miezi kadhaa ya karibuni katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan hasa katika miji ya Jenin na…

Onyo la Tel Aviv kwa Wazayuni kuhusu safari ya kwenda nchini Qatar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia

Onyo la Tel Aviv kwa Wazayuni kuhusu safari ya kwenda nchini Qatar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia

Makao makuu ya utawala wa Kizayuni yamewashauri wakazi wa maeneo hayo yanayokaliwa kwa mabavu kutosafiri hadi Qatar kutazama michezo ya Kombe la Dunia kutokana na vitisho vya usalama. Wakati wa michezo ya Kombe la Dunia inayofanyika nchini Qatar, Makao Makuu ya Kupambana na Ugaidi ya Kizayuni jana (Jumapili) yalitoa taarifa na kuwashauri Wazayuni wasisafiri kwenda…

Hamas: Israel isichukue hatua ya kijinga dhidi ya wafungwa

Hamas: Israel isichukue hatua ya kijinga dhidi ya wafungwa

“Kataib Ezzedin al-Qassam”, tawi la kijeshi la harakati ya Hamas nchini Palestina, lilitoa onyo kwa utawala wa Kizayuni kwamba haupaswi kufanya ujinga kwa kuwalenga wafungwa. “Kataib Izzedin al-Qassam”, tawi la kijeshi la harakati ya Hamas nchini Palestina, siku ya Alkhamisi, liliuonya utawala wa mpito wa Kizayuni kwamba harakati hiyo itatumia juhudi zake kumlazimisha adui akubali…

Pigo jingine kwa Wazayuni, Morocco yasherehekea kwa bendera ya Palestina, kupanda Kombe la Dunia

Pigo jingine kwa Wazayuni, Morocco yasherehekea kwa bendera ya Palestina, kupanda Kombe la Dunia

Katika hali ambayo serikali ya Morocco imetangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu na ya Waislamu, wamezidi kuonesha kutokubaliana na uamuzii huo wa utawala wa kifalme wa Morocco. Baada ya kufanikiiwa kupanda kwenye awamu ya mtoano ya mashindano ya Kombe la Dunia la Kandanda 2022 yanayoendelea…