Abbas: Haina maana kuwa na nchi ya Palestina bila ya Quds, Gaza na Ukingo wa Magharibi
Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesisitiza kuwa, haitakuwa na maana yoyote kuwa na nchi ya Palestina bila ya Baitul Muqaddas (Jerusalem), Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Abbas, ameyasema hayo katika hotuba aliyotoa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 18 wa kifo cha Yasser Arafat, Rais wa zamani…
Uchochezi wa Netanyahu dhidi ya Iran katika mahojiano na “Shultz”
Katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Ujerumani, mkuu wa Chama cha Likud alizungumza kuhusu tishio la mpango wa nyuklia wa Iran dhidi ya Tel Aviv. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa, Waziri Mkuu wa Ujerumani amempongeza “Benjamin Netanyahu” kwa ushindi wa kiongozi wa chama cha Likud cha utawala wa muda…
Ripoti: Tel Aviv inatumia “mbinu za kimafia” dhidi ya makundi ya haki za binadamu ya Palestina
Shirika la kutetea haki za binadamu la Palestina limesema katika ripoti yake kwa kamati ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kwamba Israel inatumia vitisho na mbinu za kimafia kuyanyamazisha mashirika ya kutetea haki za binadamu. Kundi la wanaharakati wa haki za binadamu wa Palestina limeiambia kamati ya Umoja wa Mataifa kwamba katika fremu ya unyanyasaji…
Kiongozi wa HAMAS: Mazingira ya Ukingo wa Magharibi ni utangulizi wa kuutokomeza utawala wa Kizayuni
Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema mazingira ya hivi sasa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni utangulizi wa kutokomezwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Mahmoud Az-Zahar ameongeza kuwa, nchi kama Syria, Lebanon na Palestina ambazo zimedhuriwa na utawala wa Kizayuni, inapasa zisimame pamoja…
Mzayuni aangamizwa katika operesheni ya wanamapambano wa Palestina
Kanali ya televisheni ya KAN ya utawala wa Kizayuni, mapema leo Jumanne imetangaza habari ya kuangamizwa mlowezi mmoja Mzayuni anayejulikana kwa jina la Shalom Sofer ambaye alijeruhiwa katika operesheni moja ya mwanamapambano wa Palestina. Televisheni hiyo imetangaza kuwa, Shalom Sofer alikuwa mlowezi wa Kizayuni anayeishi katika kitongoji cha Kedumim cha walowezi wa Kizayuni kilichojengwa kwenye ardhi…
Jordan yaonya kuhusu hatua za Israel za kuzusha mizozo Palestina
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jordan ameonya kuhusiana na hatua za utawala haramu za Israel za kuzusha mivutano na mifarakano dhidi ya Wapalestina. Ayman Safadi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jordan amesema hayo katika mazungumzo yake na mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa katika mwenendo wa amani ya Asia Magharibi na kutahadharisha kuhusiana…
Bahrain: Tunataka mahusiano yetu na Israel yawe yenye kupigiwa mfano
Mshauri wa mfalme wa Bahrain amesema, nchi hiyo itaendeleza uhusiano wake na utawala wa Kizayuni katika kipindi cha aliekua waziri mkuu Bw. Netanyahu. “Khalid bin Ahmed Al Khalifa”, waziri wa zamani wa mambo ya nje na mshauri wa sasa wa Mfalme wa Bahrain katika masuala ya kidiplomasia, alisema kuwa Manama itaendeleza uhusiano wake na utawala…
Vyombo vya habari vya Israel: Miaka 25 ijayo, utawala wa Kizayuni utakuwa umeshatoweka
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa Israel yanaonyesha kuwa theluthi moja ya walowezi wa Kizayuni hawataki kuajiriwa jeshini na wanaamini kuwa nchi iitwayo Israel haitakuwepo tena baada ya miaka 25. Kwa mujibu wa televisheni ya Al-Mayadeen, baadhi ya vyombo vya habari vya Israel vimefichua kuwa thuluthi moja ya vijana wa Israel hawaamini kama Israel itakuwepo…