Iran: Israel inapaswa kuharibu silaha zake za nyuklia na ijiunge na NPT
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel uharibu silaha zake za nyuklia na ujiunge haraka na Mkataba za Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT). Majid Takht Ravanchi alisema hayo katika Mkutano wa Kumi wa Kuangalia Upya Maazimio ya Nchi…
HAMAS yasisitizia msimamo wake wa kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na Wazayuni
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kwa mara nyingine tena imesisitiza kwamba, inapinga kuanzishwa uhusiano wa aina yoyote na utawala haramu wa Israel. Taarifa iliyotolewa na Kituo cha Upashaji Habari cha Palestina imeeleza kuwa, HAMAS inakanusha madai ya baadhi ya vyombo vya habari kwamba, imeafiki suala la kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Uturuki…
HAMAS: Jukumu la kambi ya muqawama ni kuifuta Israel katika uso wa dunia
Kiongozi mmoja mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, jukumu kuu la kambi ya muqawama ni kuhakikisha ardhi zote za Palestina zinakombolewa na hiyo maana yake ni kufutwa katika uso wa dunia, utawala pandikizi wa Kizayuni ambao unazikalia kwa mabavu ardhi za Palestina. Shirika la habari la FARS limemnukuu Mahmoud…
Nasrullah: Ushindi wa mwaka 2000 wa Muqawama ulitamatisha mradi wa “Israel Kubwa”
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, ushindi wa mwaka 2000 wa Muqawama ulihitimisha mradi wa “Israel Kubwa.” Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema hayo katika hotuba ya ufungaji wa sherehe za kuadhimisha “Machipuo Arubaini” kwa mnasaba wa kutimia miaka 40 tangu ilipoasisiwa harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah. Nasrullah ameeleza kuwa kuna mafungamano makubwa baina ya…
Wanajeshi wa Israel waendeleza jinai katika maeneo tofauti ya Palestina
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wanaendelea na jinai zao dhidi ya Wapaelstina katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kanali ya Telegram ya al Risala imesambaza mkanda wa video leo Jumanne unaoonesha jinai za wanajeshi makatili wa Israel na jinsi wanavyovamia na kufanya ukatili dhidi ya Wapalestina katika mji wa al Khalil wa…
Zaidi ya nusu karne sasa tangu kufanyika jinai ya kuchomwa moto Msikiti wa al-Aqswa
Jumapili ya jana tarehe 21 Agosti ilisadifiana na kutimia mwaka wa 53 tangu kuchomwa moto Msikiti mtakatifu wa al-Aqswa, kibla cha kwanza cha Wiaslamu, jinai ambayo ilifanywa na utawala vamizi wa Israel ambapo walimwengu walibakia kuwa watazamaji tu na kutoonyesha radiamali yoyote kwa kitendo hicho cha kinyama. Tarehe 21 Agosti 1969 Mzayuni mmoja aliuchoma moto…
Wafungwa wa Palestina waanza mgomo wa kula
Mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel wameanzisha mgomo usio na kikomo wa kula chakula. Shirika la habari la Palestin al-Yaum limeinukuu Bodi ya Wafungwa Wapalestina ikisema kuwa, hali ya taharuki imetanda katika jela na magereza ya utawala wa Kizayuni, baada ya mateka hao wa Kipalestina kuanza mgomo…
Siku ya Kimataifa ya Misikiti; Palestina iko mstari wa mbele kulinda Msikiti wa al Aqsa
Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa katika mji mtakatifu wa Quds huko Palestina amesema kuwa, Msikiti huo mtakatifu bado uko kwenye moto wa jinai za Wazayuni lakini wananchi wa Palestina wataendelea kuwa mstari wa mbele kuulinda. Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ya Palestina OIC imeitangaza tarehe 21 Agosti kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Misikiti…