HAMAS: Muqawama una uungaji mkono mkubwa wa Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi
Kiongozi mmoja mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiisalamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, muqawama uko chini ya mwavuli wa uungaji mkono wa kivitendo wa Wapalestina na jambo hilo ndilo linalozidi kutia nguvu harakati za muqawama katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kituo cha upashaji habari cha Palestina kimeripoti habari hiyo na kunukuu matamshi…
Wapalestina wa Gaza wataka kushtakiwa Wazayuni walioua watoto wao
Wakazi wa Ukanda wa Gaza wamefanya maandamano wakitaka kufunguliwa mashitaka utawala wa Kizayuni wa Israel katika mahakama za kimataifa, kwa kuua watoto wa Kipalestina katika eneo hilo ambalo liko chini mzingiro. Wakazi wa Gaza, familia na jamaa za watoto wa Kipalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya hivi karibuni ya jeshi katili la utawala haramu wa…
Marekani inaiba 80% ya mafuta yanayozalishwa Syria kila siku
Marekani inapora asilimia 80 ya mafuta yanayozalishwa kwa siku nchini Syria. Wizara ya Mafuta ya Syria imesema vikosi vamizi vya Marekani vinaiba mapipa 66,000 za mafuta ghafi kwa siku katika nchi hiyo ya Kiarabu. Kwa mujibu wa wizara hiyo, kiwango hicho kinachoibiwa na wanajeshi vamizi wa Marekani katika nch hiyo inayoshuhudia vita tangu mwaka 2011,…
HAMAS: Muqawama ndio njia bora kabisa ya kuikomboa ardhi ya Palestina
Mjumbe mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, muqawama na mapambano ndio njia bora kabisa ya kuzikomboa ardhi za Palestina na kuifanya Palestina kuwa huru. Ismail Ridhwan amesisitiza kuwa, jibu la Wapalestina kwa jinai za utawala ghasibu wa Israel unaokalia Quds kwa mabavu litakuwa ni mtutu wa bunduki. Kiongozi huyo…
Israel yakiri kuwaua watoto Wapalestina Gaza
Utawala wa Kizayuni wa Israel umekiri kuwaua watoto watano Wapalestina katika hujuma yake ya hivi karibuni dhidi ya Ukanda wa Gaza. Utawala huo dhalimu ulianzisha vita dhidi ya Gaza mnamo Agosti 5 na vita hivyo vilimalizika baada ya siku tatu kufuatia upatanishi wa Misri. Jumla ya watu 49 waliuawa shahidi katika hujuma hiyo ya Israel…
Kukiri Mkuu wa Sera za Nje wa EU kwamba Magharibi imeonyesha undumakuwili katika kadhia za Ukraine na Gaza
Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amekiri kuwa nchi za Magharibi zinatumia vipimo vya nyuso mbili na za undumilakuwili kuhusiana na masuala ya kimataifa. Akijibu suali aliloulizwa katika moja ya mahojiano aliyofanyiwa, kuhusu msimamo wa Umoja wa Ulaya kwa watu wa Ukraine na Gaza; pamoja na Borrell kukiri kuwa vimetumika vipimo vya…
DAESH (ISIS) wametumia asilimia 90 ya silaha za Marekani katika operesheni za kigaidi
Mtaalamu mmoja wa masuala ya kiusalama amesema, asilimia 90 ya wahanga na waathirika wa ugaidi nchini Iraq hasa katika maeneo yaliyokombolewa wameuliwa kwa silaha za Marekani. Japokuwa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh limeshindwa na kusambaratishwa katika nchi za Iraq na Syria, mabaki ya magaidi wa kundi hilo yangaliko katika nchi hizo na Marekani…
Kani: Israel inakoseshwa usingizi na kizazi kipya cha Wapalestina
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema kuwaua watoto wa Kipalestina kumegeuka na kuwa jambo la kawaida kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, na umwagaji damu huo unadhihirisha wazi kuwa Wazayuni wanakiogopa kizazi kipya cha Wapalestina. Ali Bagheri Kani alisema hayo jana hapa Tehran katika mazungumzo yake na Mohammed bin Abdulaziz al-Khulaifi,…