Wamagharibi wakosolewa kwa undumakuwili juu ya vita Ukraine na Gaza
Harakati inayopinga dhulma na ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina imekosoa vikali undumakuwili wa nchi za Magharibi kuhusu vita nchini Ukraine kwa upande mmoja na katika Ukanda wa Gaza, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa upande mwingine. Harakati ya Kimataifa ya Kuususia Utawala haramu wa Israel BDS katika taarifa jana Jumamosi…
Ghalibaf: Muqawama wa Palestina umetoa bishara ya kuangamia utawala wa Kizayuni
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, muqawama na mapambano ya harakati ya Jihad al Islami ya Palestina mbele ya utawala wa Kizayuni wa Israel yametoa bishara njema ya kuangamia utawala huo pandikizi. Shirika la habari la IRNA limemnkuu Mohammad Bagher Ghalibaf akisema hayo leo katika kikao cha wazi cha Bunge…
Wazayuni 10 walijeruhiwa kwa kupigwa risasi katika mji wa Jerusalem unaokaliwa kimabavu
Polisi ya Kizayuni imetangaza kuwa, Wazayuni 10 walijeruhiwa katika shambulizi la asubuhi katika basi moja mjini Jerusalem inayokaliwa ki mabavu. Shirika la habari la Palestina la Shahab limeripoti kuwa wapiganaji wa makundi ya muqawama waliwafyatulia risasi Wazayuni waliokuwa kwenye kituo cha mabasi huko mjini Jerusalem. Kanali ya habari ya Elium ya Urusi imeripoti kuwa Wazayuni…
Wanamichezo Wairaq wakataa kupambana na timu ya Israel katika mashindano ya Romania
Wanamichezo wawili Wairaqi wa mchezo wa tenisi wamekataa kupambana na wanamichezo kutoka utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika michuano ya Paralampiki inayofanyika nchini Romania. Wanamichezo wengi wanaounga mkono Palestina katika nchi za Kiislamu na Kiarabu hawautambui utawala wa Kizayuni na hawako tayari kupambana na wapinzani wao wanaowakilisha Israel katika mashindano mbalimbali ya michezo. Tovuti…
HAMAS yapongeza misimamo ya waziri wa ulinzi wa Pakistan dhidi ya Israel
Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amepongeza msimamo thabiti ulioonyeshwa na waziri wa ulinzi wa Pakistan dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Waziri wa ulinzi wa Pakistan Khawaja Muhammad Asef ameieleza serikali ya Uingereza na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo kuwa Azimio la Balfour la mwaka…
Israel imewaua shahidi watoto Wapalestina zaidi ya 1,000 tangu 2008
Tangu mwaka 2008, zaidi ya watoto elfu moja wa Kipalestina wameuawa shahidi katika Ukanda wa Gaza katika mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya Al-Mayadeen siku ya Alkhamisi, mashahidi 15 kati ya 43 wa mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza…
Jibu la Kiongozi Muadhamu kwa Barua ya Katibu Mkuu wa Jihad Islami ya Palestina
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu barua ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na kusema, “mapambano (muqawama) ya kishujaa ya Jihad Islami yatapelekea kupanda hadhi ya harakati hii katika mapambano sambamba na kusambaratisha hadaa za utawala wa Kizayuni na kuufedhehesha utawala huo.” Kwa mujibu wa taarifa ya tovuti ya Ofisi…
Je, ni nani mshindi hasa wa vita vya siku tatu huko Gaza?
Ikiwa ni katika kueneza siasa zake za kipropaganda, utawala wa Kizayuni wa Israel unaeneza uongo kuwa mara hii harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS haikushirikiana na harakati ya Jihad Islami katika vita vya siku tatu vya hivi karibuni huko Katika Ukanda wa Gaza. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba utawala huo unapuuza kwa…