
Afrika Kusini: Sasa ni wakati wa kuikomboa Palestina
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Afrika Kusini, Zain Dangore, alitoa wito wa kuhamasishwa kwa njia zote za kuwakomboa Wapalestina kutoka katika uvamizi wa Utawala wa Kizayuni. “Ni lazima kuhamasisha kila njia kwa ajili ya ukombozi wa Palestina”; Hili ni pendekezo la afisa huyo mkuu wa Afrika Kusini kumaliza uvamizi wa Israel….

Misri yajiunga na Afrika Kusini katika kuwasilisha malalamishi yao dhidi ya Israel katika Mahakama ya The Hague
Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri sambamba na kutangaza uungaji mkono wake kwa malalamiko ya Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu dhidi ya mauaji ya Israel katika Ukanda wa Gaza, imesisitiza kuwa, mashambulizi ya Israel yamesababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu ambao haujawahi kushuhudiwa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri iliunga mkono…

Waisraeli wanne wafukuzwa kutoka kwenye hoteli moja nchini Tanzania kwa kulalamika kuhusu ‘Sticker’ yenye maandishi ya “free palestine” yaliyokua kwenye gari la meneja
Hoteli ya Canary nungwi mjini Zanzibar iliwatimua Waisraeli wanne waliomhoji mhudumu aliyekua katika sehemu ya mapokezi ya wageni kuhusu gari lililokuwa nje ya jengo hilo lililokua na stika zenye maandishi ya “free palestine”. Waisraeli hao walielezwa kwamba gari hilo ni la meneja wa hoteli hiyo, na hatimaye walifukuzwa baada ya kulalamika kuwa gari hilo liliwapa…

Sputnik: Majibu ya adhabu ya Iran yalifichua udhaifu wa kijeshi wa Israel / Iran ina ramani kamili ya mifumo ya makombora ya Israel
Akirejelea jibu la kuadhibu la Iran kwa mashambulizi ya kichokozi ya utawala wa Kizayuni, mchambuzi wa Sputnik alibainisha: kiwango cha hatua ya Iran kiliilazimisha Israel kupeleka teknolojia yake na ya Marekani ya kukabiliana na makombora katika eneo zima; Iran sasa ina “ramani kamili ya mfumo wa ulinzi wa makombora wa Israeli” katika milki yake. Kwa…

Mchambuzi wa Algeria: Kama isingekuwa Iran, Israel ingeteka nchi zote za Kiarabu
Mchambuzi wa Algeria sambamba na kupongeza mashambulizi ya adhabu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya misimamo ya utawala wa Kizayuni katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu, alizishambulia nchi za maelewano ya Kiarabu na kuzitaja kuwa ni “wafuasi na waungaji mkono wa adui mkubwa wa Waarabu na Waislamu”. Kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sheria za…

Ujumbe wa utawala wa Israel kwa Marekani: “Ni Lazima tujibu mashambulizi ya Iran; Lakini tutahitajia ushirikiano wenu”
Baadhi ya vyombo vya habari vya Kizayuni viliripoti kwamba ujumbe wa Israel kwa Marekani unasisitiza uhakika wa jibu kwa ushirikiano kamili wa Marekani. Vyombo vya habari vya Kizayuni vilisisitiza kuwa ujumbe wa Israel kwa Marekani ni kwamba ni lazima tuijibu Iran, lakini tutafanya hivyo kwa ushirikiano wenu. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kizayuni,…

Kumalizika kwa mkutano wa baraza la vita la utawala wa Israel bila ya uamuzi juu ya jibu kwa Iran
Mkutano wa baraza la vita la utawala wa Israel ulimalizika bila ya uamuzi wa jinsi ya kujibu Iran. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, CNN imewanukuu maafisa wa utawala wa Kizayuni na kutangaza kuwa: “Kikao cha Baraza la Vita vya Israel kilimalizika bila ya kuwepo uamuzi wa namna ya kujibu mashambulizi ya Iran.” Kwa mujibu wa…

Makubaliano kati ya utawala wa Kizayuni na Indonesia ili kurekebisha uhusiano
Baada ya miezi mitatu ya mazungumzo ya siri kati ya Indonesia na utawala wa Kizayuni, pande hizo mbili zilifikia makubaliano ya kurejesha uhusiano wa kawaida na ushirikiano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OCDE). Makubaliano hayo ni sehemu ya juhudi za kuwezesha Indonesia kujiunga na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OCDE),…