
Waziri wa Kizayuni: Sielewi wasiwasi wa polisi kuhusu bendera ya Palestina!
Waziri wa Ushirikiano wa Kieneo wa Kizayuni katika mazishi ya marehemu mwandishi wa habari wa Al-Jazeera, amesema kuwa mienendo ya jeshi la Kizayuni ni utovu wa kimaadili na haelewi sababu ya wao kuogopa bendera ya Palestina. Kwa mujibu wa Fars News, Waziri wa Ushirikiano wa Kieneo wa Israel Issawi Frij alikosoa mienendo ya jeshi la…

Haaretz: Jeshi la Israel lakiri mauaji ya Shirin Abu Aqla
Jeshi la Israel limekiri kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Al-Jazeera katika mji wa Jenin baada ya kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel kulingana na uchunguzi uliofanyika kuhusu mauaji ya mwanahabari huyo. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Fars, licha ya madai ya maafisa waandamizi wa utawala wa muda wa Kizayuni kwamba…

Jordan: Masjidul-Aqswa ni mali ya Waislamu, Israel yatakiwa kutoitahini subira ya Waislamu bilioni 2
Kamati ya Palestina katika Bunge la Jordan imesisitiza kuwa, Waislamu wana mamlaka mutlaki kwa msikiti mtakatifu wa al-Aqswa ulioko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Kamati hiyo imeuonya utawala ghasibu wa Israel na kuutaka usiitahini subira ya Waislamu bilioni 2 ulimwenguni. Msimamo huo wa Kamati ya Palestina katika Bunge la Jordan umetolewa kufuatia matamshi ya Naftali Bennett, Waziri…

Sherehe za kuanzishwa kwa utawala wakimabavu mjini Abu Dhabi zaashiria kudhoofika kwa watawala wa UAE.
Chama cha People’s Front for the Liberation of Palestina kimeelezea sherehe za kumbukumbu ya kuasisiwa utawala huo ghasibu katika ubalozi wake mjini Abu Dhabi kuwa ni ishara ya kudorora na kudhalilika kwa watawala wa Imarati. Kwa mujibu wa Huduma ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars, Chama cha People’s Front for the Liberation of…

Mmoja auawa na polisi nchini Nigeria katika maandamano ya Siku ya Al-Quds Duniani
Polisi wa Nigeria wamemuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa katika shambulizi lililofanywa dhidi ya waandamanaji wa Siku ya Al-Quds Duniani huko Zaria, Jimbo la Kaduna. Takriban mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati polisi walipowafyatulia risasi wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) wakati wa maandamano ya Siku ya Dunia ya Al-Quds…

Kiongozi Muadhamu: Kuhudhuria kwa wananchi katika maandamano ya leo ni utetezi wa kweli wa Al-Quds / Mipango ya mapatano na Wazayuni imebatilishwa / Kipofu hawezi tena kuwa kipofu!
Katika Hotuba yake ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Ali Khamenei alizungumza katika siku hii inayosadifiana na Siku ya Kimataifa ya Quds iliyorushwa moja kwa moja na kupitia televisheni akisema; ‘Salamu kwa taifa lao kuu la Iran, ambalo limeunda historia siku hii ya…

Maandamano ya Siku ya Quds Duniani yafanyika mjini Tehran yakihudhuriwa na watu mbali mbali wenye matabaka tofauti kutoka kote nchini.
Kwa mujibu wa ripoti hii, mwaka huu, baada ya mapumziko ya miaka miwili ya kufanya maandamano ya hadhara ya Siku ya Quds Duniani kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona, uratibu wa kimsingi ulifanyika ili kuandaa maandamano makubwa yatakayofanyika kwa wakati mmoja sawia na maandamano ya mji wa Tehran, katika zaidi ya miji 900. Maandamano…

Mkutano wa Jordan na Israel wa kukagua Msikiti wa Al-Aqsa
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni viliripoti kikao cha maafisa wa utawala huo na viongozi wa Jordan baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kulenga Msikiti wa Al-Aqsa. Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa, kikao cha wakuu wa Jordan na Israel kuhusu Msikiti wa Al-Aqsa kitafanyika kwa kiwango cha juu zaidi. Tovuti ya…