Ziara ya kiduru ya Lavrov katika nchi za Afrika; jitihada za Russia za kuzidisha satwa yake barani Afrika
Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Jumatatu tarehe 23 mwezi huu alianza safari ya kiduru kwa kuzitembelea nchi kadhaa za Kiafrika na hadi sasa amefanya safari huko Afrika Kusini, Eswatini, Angola na Eritrea. Hii ni safari ya pili kufanywa na Lavrov barani Afrika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Waziri wa Mambo…
Jihadul-Islami: Misimamo ya Uturuki na UAE kuhusu operesheni ya Quds ni usaliti kwa Palestina
Mkuu wa ofisi ya habari ya harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesema, misimamo ya Uturuki na Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) ya kulaani operesheni ya kujitolea kufa shahidi iliyotekelezwa katika mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu ni usaliti kwa watu wa Palestina. Wizara za mambo ya nje za Uturuki na Imarati (UAE) zimetoa…
Mahakama ya Mali yamhukumu kifo mtu mmoja kwa vifo vya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa
Mahakama nchini Mali imemhukumu kifo mwanaume mmoja kwa kuhusika katika shambulio mwaka 2019 lililouwa wanajeshi watatu wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa. Hayo yameelezwa na kikosi cha kulinda amani cha UN nchini Mali (MINUSMA) Mali ambayo inaongozwa na serikali ya kijeshi kwa muongo sasa imekuwa ikipambana na hali ya mchafukoge inayosababishwa na makundi yanayobeba…
Paris yamwita nyumbani balozi wake baada ya wanajeshi wake kutimuliwa Burkina Faso
Baada ya serikali ya Burkina Faso kuiamuru Ufaransa iondoe wanajeshi wake katika kipindi cha mwezi mmoja ujao, mkoloni huyo kizee wa Ulaya amehamakishwa na hatua hiyo na ameamua kumrudisha nyumbani balozi wake kutoka Ouagadougou. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Fars, siku moja baada ya Ufaransa kusema kuwa itaheshimu uamuzi…
Vifo vya kimbunga cha tropiki cha Cheneso vyaongezeka nchini Madagascar
Idadi ya vifo imeongezeka na kufikia watu 16 huku watu wengine 19 wakiwa bado hawajulikani walipo baada ya dhoruba kali ya kimbunga cha tropiki iliyopewa jina la Cheneso kuipiga Madagascar. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya jana Alkhamisi iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Kudhibiti Hatari na Majanga ya nchi hiyo, (BNGRC). Taarifa ya…
Mgogoro wa nishati Ulaya na kukimbilia Italia kwenye gesi ya Algeria
Waziri Mkuu wa Italia, Bi Giorgia Meloni Jumatatu wiki hii alifanya ziara ya siku mbili nchini Algeria na kutia saini mikataba kadhaa ya kuongeza kiwango cha kuingia barani Ulaya gesi nyingi zaidi ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanywa kwa pamoja baina ya Waziri Mkuu wa Italia Giorgia…
Taasisi za haki za binadamu zaidi ya 170 zataka kuhitimishwa maafa ya binadamu Yemen
Mashirika na taasisi za haki za binadamu za kimataifa zaidi ya 170 zimetaka kuhitimishwa maafa ya binadamu huko Yemen na mzingiro dhidi ya nchi hiyo. Kwa uungaji mkono wa Marekani, Muungano wa Falme za Kiarabu na nchi nyingine kadhaa, Saudi Arabia iliivamia kijeshi Yemen mwezi Machi 2015 na kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya nchi kavu, baharini…
Onyo la Herzog la kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya utawala wa Kizayuni
Mizozo na migogoro imeongezeka ndani ya utawala wa Kizayuni kiasi kwamba, rais wa utawala huo pandikizi, Isaac Herzog ametishia tena kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe na hali ya Israel kuripuka kutokana na mizozo ya kisiasa na mifarakano shadidi katika jamii ya utawala wa Kizayuni. Baraza jipya la mawaziri la Benjamin Netanyahu ambalo ni baraza…