Vyombo vya Habari

Israel yaufyata baada ya onyo la Russia, yakataa ombi la US la kuipa Ukraine makombora

Israel yaufyata baada ya onyo la Russia, yakataa ombi la US la kuipa Ukraine makombora

Utawala haramu wa Israel umepinga ombi la Marekani la kuutaka uipe Ukraine makombora na silaha nyinginezo, baada ya Russia kuonya vikali dhidi ya kupewa Kiev misaada ya kijeshi na zana za vita. Tovuti ya Russia Today imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, duru za habari zimenukuliwa na shirika la habari la Axio zikisema kuwa, Israel…

Siku ya umwagaji damu katika kambi ya Jenin; kilele cha misimamo mikali ya baraza la mawaziri la Netanyahu

Siku ya umwagaji damu katika kambi ya Jenin; kilele cha misimamo mikali ya baraza la mawaziri la Netanyahu

Ikiwa ni katika kuendeleza ugaidi na jinai dhidi ya Wapalestina wasio na hatia, Alkhamisi asubuhi, baraza la mawaziri lenye misimamo mikali ya kupindukia mipaka la utawala wa Kizayuni lilitekeleza jinai nyingine ya kutisha dhidi ya Wapalestina wanaoishi katika kambi ya wakimbizi huko Jenin. Jana asubuhi, askari wa utawala wa Kizayuni huku wakisaidiwa moja kwa moja…

Iran na Tanzania zahimiza ushirikiano zaidi baina yao hasa katika uwekezaji viwandani

Iran na Tanzania zahimiza ushirikiano zaidi baina yao hasa katika uwekezaji viwandani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Tuko tayari kutoa ujuzi na uzoefu wetu, hasa katika nyanja za elimu, kilimo, uvuvi, ujenzi wa mabwawa, usimamizi wa vyanzo vya maji na kilimo umwagiliaji, ili kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za mapinduzi ya viwanda. Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Hossein Amir-Abdollahian na “Stergomena Lawrence…

Raisi: Uhusiano wa Iran na Syria umejengeka katika misingi ya muqawama

Raisi: Uhusiano wa Iran na Syria umejengeka katika misingi ya muqawama

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uhusiano wa Iran na Syria ni thabiti na kwamba umejengwa katika misingi ya moyo wa muqawama na mapambano ya wananchi wa mataifa haya mawili. Sayyid Ebrahim Raisi alisema hayo jana Jumanne hapa Tehran katika mazungumzo yake na Ali Mahmoud Abbas, Waziri wa Ulinzi wa Syria na kusisitiza kuwa, Tehran…

Rwanda yashambulia ndege ya kivita ya DRC kwa ‘kukiuka’ anga yake

Rwanda yashambulia ndege ya kivita ya DRC kwa ‘kukiuka’ anga yake

Serikali ya Kigali imesema imechukua ‘hatua za kujilinda’ baada ya ndege ya kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kukiuka anga ya Rwanda. Yolande Makolo, Msemaji wa Serikali ya Rwanda amesema katika taarifa kuwa, ndege ya kijeshi ya Sukhoi-25 ya DRC jana Jumanne adhuhuri ilikiuka anga ya Rwanda kwa mara ya tatu sasa, na kwamba Kigali…

Lissu arejea nyumbani kwa kishindo; ujio wake utahuisha upinzani Tanzania?

Lissu arejea nyumbani kwa kishindo; ujio wake utahuisha upinzani Tanzania?

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amerejea nyumbani kutoka uhamishoni baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa marufuku ya mikutano ya kisiasa ya hadhara. Lissu amewasili leo Jumatano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Ubelgiji, na kupokea viongozi, wanachama na mamia ya wafuasi wa Chama cha upinzani cha Chadema. Jeshi la polisi…

Mashirika ya kimataifa yatiwa wasiwasi na mgogoro wa chakula barani Asia

Mashirika ya kimataifa yatiwa wasiwasi na mgogoro wa chakula barani Asia

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na taasisi nyingine za Umoja wa Mataifa zimeripoti kuwa, idadi kubwa ya wakazi wa bara Asia hawana chakula cha kutosha kufautai kuongezeka ukosefu wa usalama wa chakula uliosababishwa na kupanda kwa bei na kuongezeka umaskini katika jamii. Russia na Ukraine zina nafasi athirifu na muhimu…

Ulaya yatiwa wasiwasi na uhaba wa dawa aina ya Antibiotic

Ulaya yatiwa wasiwasi na uhaba wa dawa aina ya Antibiotic

Maafisa wa Afya wa Kamisheni ya Ulaya wamelazimisha kuitisha mkutano kufuatia nchi za bara hilo kukumbwa na ukosefu wa dawa aina ya antibiotic. Nchi za Ulaya  ambazo zinaendelea kutatizwa na ugonjwa wa Uviko-19 na magonjwa mengine katika msimu huu wa baridi kali hivi sasa zinakabilwia na ukosefu mkubwa wa dawa khususan zile za antibiotioc kutokana…