Umoja wa Mataifa walaani kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu nchini Sweden
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu (kitabu kitakatifu cha Waislamu) nchini Sweden. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza msimamo huo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu nchini Sweden na akasema:…
Kuanza tena uchunguzi kuhusu mlipuko wa bandari ya Beirut
Duru za habari za Lebanon zimetangaza kuwa hakimu anayechunguza kesi ya mlipuko uliotokea mwaka 2020 katika bandari ya Beirut ameamua kuanzisha tena uchunguzi wa kesi hiyo. Tareq Al-Bitar hakimu anayechunguza mlipuko katika bandari ya Beirut ameamua uchunguzi kuhusiana na kesi hiyo uanzishwe tena. Baadhi ya duru za habari zimearifu kuwa, al Bitar ameamua kuwasilisha kesi mahakamani dhidi…
Mtazamo mwingine kuhusu uwekezaji mkubwa wa Bin Salman katika michezo Saudia
Iwapo mtu yeyote atafuatilia habari za Saudi Arabia baada ya kunyakuliwa madaraka ya nchi hiyo ya kifalme na Mohammed bin Salman, atakumbana na mkanganyiko mkubwa katika mielekeo na sera za nchi hiyo. Moja ya matukio na mifano ya wazi katika uwanja huo ni kwamba, kwa upande mmoja, Bin Salman anataka kuonyesha sura inayoitwa ya kisasa…
Maandamano makubwa ya wananchi wa Yemen kulaani uhalifu wa kuchoma Qur’ani nchini Uswidi
Wananchi wa Yemen walifanya maandamano makubwa katika uwanja wa Bab El-Iman huko Sana’a Jumatatu hii jioni kulaani uhalifu wa kuchoma Quran nchini Uswidi. Washiriki hao walionyesha hasira na kuchukizwa kwao kwa kuyatusi maeneo matukufu ya Kiislamu na kutaka kuchukua misimamo mikali ili kukomesha mashambulizi hayo ya mara kwa mara dhidi ya maeneo matukufu ya Kiislamu….
Shirika la hisani lasambaza Misahafu 11,000 barani Afrika
Taasisi ya kutoa misaada ya Uturuki ilitoa zaidi ya nakala 11,000 za Misahafu (Qur’ani Tukufu) kwa Waislamu katika nchi tofauti za Kiafrika mwaka jana. Wakfu wa Misaada ya Kibinadamu au IHH imesambaza Misahafi hiyo katika nchi za Nigeria, Mali, Burkina Faso, Chad, Guinea, Ethiopia, Benin na Sudan. Taasisi hiyo ilisema katika taarifa yake kwamba, kwa…
Mwanasiasa wa upinzani Eswatini auawa kwa kupigwa risasi
Watu wenye silaha nchini Eswatini wamemuua kwa kumpiga risasi mwanasiasa mashuhuri wa upinzani na ambaye pia alikuwa mwanasheria wa haki za binadamu. Hayo yameelezwa na msemaji wa chama chake ambaye ameziambia duru za habari, saa chache baada ya mfalme wa nchi hiyo kuwashutumu wanaharakati wanaopinga utawala wake. Thulani Maseko aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake…
Bunduki 9,300 zimenaswa katika machafuko ya karibuni nchini Iran
Msemaji wa Kamandi ya Polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa silaha 9,300 zimekamatwa wakati wa machafuko yaliyozuka hapa nchini hivi karibuni. Kuanzia mwishoni mwa Septemba 2022, baadhi ya maeneo ya Iran yalikumbwa na machafuko; na katika siku zake za kwanza kabisa ilidhihirika wazi kuwa baadhi ya vyombo vya habari vina mkono katika kushamirisha…
Kuendelea uingiliaji hasi wa Marekani katika masuala ya ndani ya Iraq
Marekani ingali inaendelea kuingilia masuala ya ndani ya Iraq kwa namna hasi, kwa kuzingatia nyenzo za mashinikizo ilizonazo mikononi mwake. Tangu mwaka 2003, Iraq imejionea enzi mpya katika siasa na muundo wake wa madaraka. Mnamo mwaka huo, Marekani iliishambulia na kuivamia kijeshi nchi hiyo na kuupindua utawala wa Kibaathi. Japokuwa tukio hilo lilihitimisha mfumo wa kidikteta…