Mashambulio ya Saudia mpakani mwa Yemen yameua watu saba na kujeruhi 91
Duru za Yemen zimeripotiwa kuwa, tangu ulipoanza mwaka mpya wa 2023 hadi sasa, watu saba wameuawa na wengine 91 wamejeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na utawala wa Saudi Arabia katika maeneo ya mpakani mwa Yemen. Kwa uungaji mkono wa Marekani, Muungano wa Falme za Kiarabu na nchi nyingine kadhaa, Saudi Arabia iliivamia kijeshi Yemen mwezi Machi 2015…
Iran na Zimbabwe kusaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Zimbabwe zinanatazamiwa kusaini hati kadhaa za makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili ndani ya wiki kadhaa zijazo. Hayo yamesemwa na Solat Mortazavi, Waziri wa Leba na Masuala ya Kijamii wa Iran katika mazungumzo yake hapa jijini Tehran jana Jumamosi na Dakta Sekai Nzenza, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zimbabwe….
Ufaransa yatakiwa iondoe jeshi lake Burkina Faso haraka iwezekavyo
Serikali ya kijeshi inayotawala Burkina Faso imeitaka Ufaransa iwaondoe wanajeshi wake katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi katika kipindi kifupi kijacho. Chanzo cha habari ndani ya serikali hiyo kimenukuliwa na shirika la habari la Reuters kikisema kuwa, wanajeshi hao wa Ufaransa wametakiwa wawe wameondoka kikamilifu nchini Burkina Faso ndani ya mwezi mmoja ujao. Haya yanajiri baada…
ICJ yapokea rasmi ombi la UN juu ya kughusubiwa ardhi za Wapalestina na Israel
Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) imepokea rasmi ombi la Umoja wa Mataifa la kutaka maoni ya ushauri kutoka kwa chombo hicho juu ya taathira za Israel kughusubu na kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina. ICJ inatazamiwa kuandaa orodha ya mataifa na mashirika ambayo yatawasilisha taarifa za maandishi kwenye mahakama hiyo iliyoko mjini Hague nchini…
Kambi ya jeshi ya Marekani yashambuliwa kwa droni nchini Syria
Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) imekiri kuwa, moja ya kambi za kistratejia za nchi hiyo huko kusini mwa Syria imeshambuliwa kwa ndege zisizo na rubani (droni). Taarifa ya jana Ijumaa ya CENTCOM imesema kambi hiyo ya kijeshi ya Marekani imeshambuliwa kwa droni katika eneo la al-Tanf, kusini mwa Syria, karibu na mipaka ya Iraq na…
Google ya Marekani kuwapiga kalamu nyekundu wafanyakazi 12,000
Alphabet, ambalo ni shirika mama la kampuni ya intaneti ya Kimarekani ya Google limetangaza kuwa litawafuta kazi wafanyakazi zaidi ya 12,000. Sundar Pichai, Afisa Mkuu Mtendaji wa Alphabet amesema katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kampuni hiyo imeshuhudia mawimbi mazito ya kimapato kutokana na mdororo wa uchumi, na kwa msingi huo wanalazimika kuwafuta kazi wafanyakazi…
Wanajeshi saba wa Somalia wauawa katika shambulio la Shabab kwenye kambi ya kijeshi
Wanajeshi saba wa serikali ya Somalia wameuawa katika shambulio la jana Ijumaa lililofanywa na genge la ukufurishaji la al Shabab kwenye kambi ya kijeshi ya mji wa Somalia uliookombolewa na jeshi la Serikali wiki hii. Wizara ya Habari ya Somalia imetangaza habari hiyo na kusema kuwa, kamanda mkuu wa kijeshi ni miongoni mwa waliouawa baada…
Waziri wa Mambo ya Nje wa Gabon afariki dunia ghafla kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri
Waziri wa Mambo ya Nje wa Gabon, Michael Moussa Adamo, amefariki dunia ghafla kwa mshtuko wa moyo wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri. Taarifa rasmi ya serikali ya Gabon imethibitisha habari hiyo ya kufariki dunia Michael Moussa Adamo ambaye alikuwa mtu wa karibu na mshirika wa muda mrefu wa Rais Ali Bongo, hata kabla ya…