Kan’ani: Jeshi la SEPAH ni chombo muhimu mno cha kupambana na ugaidi duniani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiisamu ya Iran amejibu hatua ya Bunge la Ulaya iliyo dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na kusisitiza kuwa, SEPAH ni chombo kikubwa na muhimu zaidi cha kupambana na ugaidi duniani. Matamshi hayo ya Nasser Kan’ani yametolewa baada ya Bunge la…
Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu Afrika Kusini yafanyika Pretoria
Toleo la 13 la mashindano ya kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Afrika Kusini yalifanyika katika mji mkuu, Pretoria. Baraza la Taifa la Qur’ani la Afrika Kusini (SANQC) liliandaa hafla hiyo iliyohudhuriwa na wahifadhi wa Qur’ani kutoka kote katika nchi hiyo. Mashindano hayo yalifanyika katika Msikiti wa Nour wa Pretoria ambapo Imamu na mhubiri wa Msikiti…
Afrika Kusini yasema BRICS inatafakari kutupilia mbali sarafu ya dola ya Marekani
Nchi za Jumuiya ya BRICS ya mataifa yanayoibukia kiuchumi inataka kutupilia mbali sarafu ya dola ya Marekani na badala yake kuunda mfumo bora wa malipo ambao hautapendelea nchi tajiri. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor katika mahojiano na Shirika la Sputnika la Russia. Kundi la BRICS linazileta pamoja…
Iran: Marekani inakiuka haki za watu wenye asili ya Afrika
Iran imesema mauaji ya hivi karibuni ya polisi wa Marekani dhidi ya mwalimu mwenye asili ya Afrika ambaye hakuwa na silaha yanadhihirisha hali mbaya ya haki za binadamu ambayo watu wasio wazungu wanakabiliwa nayo kote Marekani. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kan’ani, aliyasema hayo katika ukurasa wake wa Twitter Jumanne,…
Wapinzani Uingereza walaani mswada wa sheria za kupiga marufuku migomo
Chama kikuu cha upinzani cha Leba cha Uingereza kimekashifu mpango mpya wa serikali wa kutunga sheria inayolenga kuzuia migomo, kikisema kuwa hatua hiyo yenye utata inafutilia mbali uhuru wa raia. Naibu kiongozi wa chama cha Leba Angela Rayner amesema wabunge wengi kutoka chama tawala cha Wahafidhina wa Conservative, wamewasilisha mswada huo na kwa njia hiyo,…
Saudia yasema inajaribu kufanya mazungumzo na Iran ili kupunguza taharuki
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwanamfalme Faisal bin Farhan Al Saud anasema ufalme huo unajaribu kutafuta njia ya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama njia bora ya kutatua tofauti, huku kukiwa na mchakato wa kidiplomasia kati ya majirani hao wawili unaolenga kurekebisha uhusiano uliodorora. Akizungumza katika jopo katika Jukwaa la…
Waziri Mkuu wa Bangladeshi: Uislamu ni dini ya amani, udugu, urafiki
Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina aliuelezea Uislamu kuwa ni dini ya amani, udugu na urafiki. Alisema wananchi wa Bangladesh watapata ujuzi wa kweli wa maadili na utamaduni wa Kiislamu kutoka kwa ‘misikiti ya kuigwa’ ambayo inafunguliwa nchini humo na halikadhalika katika vituo vya kitamaduni vya Kiislamu ambavyo vitawasaidia kutopotoshwa kwa jina la dini. Alisema,…
Nchi 90 zaitaka Israel kukomesha hatua za adhabu dhidi ya Wapalestina uamuzi wa ICJ ukisubiriwa
Zaidi ya nchi 90 zimeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kuacha hatua za kuwaadhibu Wapalestina kufuatia ombi la Umoja wa Mataifa la kutaka maoni ya ushauri kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ). Mwishoni mwa mwezi Desemba, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwa kupitisha azimio, lilitaka maoni ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa…