Ukurasa mwingine wa maafa ya binadamu huko Yemen; wagonjwa elfu tano wanaohitaji huduma ya Dialysis wanakaribia kuaga dunia
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen Anayehusika na Masula ya Tiba ameeleza kuwa maisha ya wagonjwa elfu tano wenye matatizo ya figo wako kwenye hatari ya kifo na Umoja wa mataifa na jamii ya kimataifa ndizo zinazopaswa kubeba dhima ya uhai na maisha ya raia hao wa Yemen. Ali…
Syria yalaani vikwazo vya kikatili vya US dhidi ya sekta ya afya ya nchi hiyo
Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeilaani vikali Marekani kwa kulenga sekta ya afya ya nchi hiyo ya Kiarabu kwa vikwazo vya upande mmoja. Katika taarifa, wizara hiyo imetoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kusimamisha vikwazo hivyo vya kikatili vya Marekani dhidi ya sekta ya afya ya taifa hilo la Kiarabu….
Iran na Zimbabwe zaazimia kupanua ushirikiano wa kimichezo
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Zimbabwe zimeazimia kupanua zaidi ushirikiano wao katikka nyanja mbalimbalii ukiwemo uga wa michezo. Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha tisa cha Kamisheni ya Pamoja ya Ushirikiano ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na taifa la Kiafrika la Zimbabwe kilichofanyika leo hapa mjini Tehran. Taarifa zaidi zinasema kuwa, imependekezwa katika…
Makumi ya wanawake watekwa na wanamgambo wenye silaha Burkina Faso
Kwa akali wanawake 50 wametekwa nyara na kundi la wanamgambo wenye silaha nchini Burkina Faso magharibi mwa Afrika. Duru za usalama zinasema kuwa, wanawake hao wametekwa nyara katika eneo la kaskazini mwa Burkina Faso ambalo limekuwa likishuhudia harakati za makundi ya waasi ambao wamehatarisha usalama na amani katika maeneo hayo. Taarifa zaidi zinasema kuwa, takriban…
Indhari ya Evo Morales kuhusu nia ya Marekani ya kufanya mapinduzi Amerika ya Latini
Evo Morales, Rais wa zamani wa Bolivia amesema kuwa, Marekani ipo katika mkondo wa kuporonmoka hasa kwa kuzingaia matukio ya hivi karibuni katika baadhi ya mataifa ya Amerika ya Latini na ni kutokana na sababu hiyo ndio maana Washington imeamua kutumia mabavu na kwamba, hivi sasa inatekeleza njama za mapinduzi katika maeneo ya Ukanda huo….
Biden atangaza hali ya maafa katika jimbo la California kufuatia mafuriko makubwa
Rais Joe Biden wa Marekani ametangaza kujiri maafa makubwa katika jimbo la California nchini humo kufuatia kimbunga mafuriko makubwa katika maeneo ambayo tayari yamejaa maji na wakati huo huo kuwepo uwezekano wa kunyesha theluji kufikia hadi mita mbili sawa na (futi sita). Jumamosi jioni Rais wa Marekani alitangaza kuwa maafa makubwa yamelikumba jimbo la California…
Indhari ya UN: Sehemu kadhaa za dunia zitashindwa kukaliwa na watu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu taathira za mabadiliko ya tabianchi kuwa, athari za ongezeko la joto duniani zitakuwa haribifu; ambapo maeneo kadhaa ya dunia yatashindwa kukaliwa na watu. Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha katika ujumbe alioutuma katika Mkutano wa 13 wa Taasisi za Kimataifa kuhusu nishati jadidika huko…
Afisa wa Ufaransa atahadharisha kuhusu hatari ya ujasusi wa Marekani barani Ulaya
Mkuu wa Kamandi ya Ulinzi wa Kimtandao wa Ufaransa ametahadharisha kuhusu hatari ya ujasusi wa Marekani kwa bara Ulaya. Jenerali Aymeric Bonnemaison Mkuu wa Kamandi ya Ulinzi wa Kimtandao ametahadharisha kuwa, ikiwa nchi za Ulaya zitaruhusu timu za ulinzi wa mtandao za Marekani kufuatilia mitandao yao, basi zitakuwa katika hatari ya kufanyiwa ujasusi na nchi…