Watu zaidi ya 40 wafariki katika ajali ya shirika la ndege la Nepal
Watu wasiopungua 44 wamefariki dunia baada ya ndege iliyokuwa imebeba watu 72 kuanguka nchini Nepal. Ndege hiyo imeanguka mapema leo ilipokuwa ikisafiri kutoka mji mkuu Kathmandu kuelekea Pokhara . Pokhara ni mji wa kitalii wenye shughuli nyingi na uko karibu kilomita 200 (maili 124) magharibi mwa Kathmandu. Sudarshan Bartaula, msemaji wa shirika la ndege la Yeti…
Wapalestina waandamana kupinga uamuzi wa kuodolewa bendera ya Palestina katika maeneo ya umma
Mamia ya Wapalestina wakazi wa Quds Mashariki huko Palestina wameandamana kulalamikia na kupinga agizo la waziri mpya wa usalama wa ndani wa utawala haramu wa Israel wa kuondolewa bendera ya Palestina katika maeneo ya umma. Wapalestina hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walisikika wakipiga nara dhidi ya Israel na waungaji mkono wake na kusisitiza kwamba,…
Mufti wa Masuni Iraq: Jinai dhidi ya makamanda wa muqawama inalazimu kulaaniwa Marekani
Mufti wa Waislamu wa madhehebu ya Kisuni nchini Iraq amelaani vikali jinai ya utawala wa Marekani ya kumuua shahidi Qassem Soleimani na Abu-Mahdi al-Mohandes na kueleza kuwa, jinai hiyo inalazimu Marekani kulaaniwa kila upande na kuchukuuliwa hatua. Sheikh Abdul-Mahdi al-Sumaidaie ameashiria jinai ya uwanja wa ndege iliyofanywa na Marekani na kubainisha kwamba, serikali ya Iraq…
Amir Abdollahian: Palestina ni suala la kwanza la ulimwengu wa Kiislamu
Hossein Amirabdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kikao na kundi la viongozi na wanachama mashuhuri wa makundi mbalimbali ya mapambano ya Palestina kwamba Palestina na Quds Tukufu bado ni suala la kwanza la ulimwengu wa Kiislamu. Hossein Amirabdollahian, akiendelea na safari yake nchini Syria, alikutana na kuzungumza…
Radiamali hasi ya Madola ya Magharibi ya kunyongwa jasusi wa Uingereza nchini Iran
Kunyongwa Ali Reza Akbari, jasusi wa shirika la kijasusi la Uingereza la MI6 kumekabiliwa na matamshi ya pupa na radiamali tofauti na hasi za madola ya Magharibi. Radiamali hizo zinaonyesha kupata pigo kubwa mipango ya kijasusi ya Magharibi dhidi ya Iran. Jumamosi ya jana tarehe 14 Januari, Idara ya Mahakama ya Iran, ilitangaza kuwa, Akbari aliyekuwa na…
Mashindano ya Qur’ani ya Bint Maktoum Yamalizika
Toleo la 23 la Mashindano ya Qur’ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum yalimalizika katika Umoja wa Falme za Kiarabu siku ya Alhamisi. Katika siku ya mwisho ya mashindano, wanaume 9 walishindana katika Ukumbi wa Tuzo la Kimataifa la Tuzo la Qur’ani Tukufu la Dubai (DIHQA) katika wilaya ya Al Mamzar ya Dubai, na wanawake…
Eneo kubwa zaidi la makaburi ya Waislamu Ulaya Magharibi lazinduliwa Uholanzi
Jumuiya ya Waislamu nchini Uholanzi imezindua makaburi makubwa zaidi ya Waislamu wa Ulaya Magharibi nchini Uholanzi. Makaburi hayo yanayoitwa Maqbara Rawdah Al Muslimin (Bustani ya Makaburi ya Waislamu), yana nafasi ya kuzikwa miili 16,000. Kwa hiyo, ni makaburi makubwa zaidi ya Kiislamu katika eneo la Ulaya Magharibi. Kulingana na Säid Bouharrou, mmoja wa waanzilishi wa…
Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu kurejea kutoka uhamishoni
Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amesema kwamba atarejea nyumbani hivi karibuni kutoka uhamishoni baada ya rais kuondoa marufuku ya mikutano ya kisiasa. Lissu, ambaye alipigwa risasi 16 katika jaribio la kutaka kumuua mwaka 2017 na amekuwa akiishi uhamishano nchini Ubelgiji, alihutubu kwa njia ya intaneti Ijumaa na kutangaza kuwa atarejea Tanzania Januari 25….