Abdollahian: Iran itaendelea kushirikiana na serikali halali ya Syria
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran itaendelea kushirikiana na serikali halali ya Syria. Hussein Amir-Abdollahian amesema hayo leo mjini Damascus mji mkuu wa Syria katika mazungumzo yake na Rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad na kusisitiza kwamba, himaya ya Tehran kwa serikali ya Syria katika kipindi chote…
Russia yadhibiti mji wa kistratajia wa Soledar, Donbass
Wizara ya Ulinzi wa Russia imesema vikosi vya jeshi la nchi hiyo vimefanikiwa kudhibiti kikamilifu mji wa kistratajia wa Soledar, ulioko katika eneo la Donbass. Eneo la Donbass lenye raia wenye asili ya Russia liko mashariki mwa Ukraine na tangu 2014 Warusi walianzisha jamhuri mbili, Donetsk na Luhansk, na kuunda serikali zilizojitenga na serikali ya…
Maonyo ya kimataifa kuhusu ukame mkali nchini Afghanistan
Maonyo makali ya kimataifa yametolewa kuhusu ukame mkali unaotokana na kushadidi baridi na kuongezeka mgogoro wa kiuchumi nchini Afghanistan. Jamii ya kimataifa inasisitiza kuwa, iwapo hali ya hivi sasa itaendelea, basi wananchi milioni 6 wa Afghanistan watakumbwa na ukame wa kuchupa mipaka. Jan Egeland, Mkuu wa Baraza la Wakimbizi la Norway ambaye hhivi karibuni alitembelea…
HAMAS: Jinai za kila uchao za Israel hazitapita hivi hivi
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) sambamba na kusema kuwa imesikitishwa na kitendo cha kuuawa shahidi vijana wawili wa Kipalestina na utawala haramu wa Israel, imeonya kuwa, jinai za kila uchao za utawala huo wa Kizayuni hazitapita hivi hivi. Taarifa iliyotolewa jana Ijumaa na HAMAS imesema kuwa, utawala ghasibu wa Israel unabeba dhima…
Lebanon yapongeza misaada, uungaji mkono wa Iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon, Abdullah Bou Habib amesifu na kupongeza misaada na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa taifa hilo la Kiarabu. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Beirut Ijumaa akiwa pamoja na Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abdullah Bou Habib amesema Lebanon inakaribisha na kuunga…
Iran yamyonga jasusi wa shirika la kijasusi la MI6 la Uingereza
Ali Reza Akbari, jasusi wa shirika la kijasusi la Uingereza amenyongwa leo nchini Iran. Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Mahakama ya Iran, Ali Reza Akbari, aliyekuwa na uraia pacha wa Iran na Uingereza, alipatikana na hatia ya kueneza ufisadi katika ardhi na kushiriki katika njama kubwa dhidi ya usalama wa ndani na wa…
Khalid Abdul Basit, mwanae qarii maarufu wa wa Misri aaga dunia
Khaled Abdul Basit Abdul Samad, mtoto wa marehemu qari maarufu wa Misri Ustadh Abdul Basit Abdul Samad alifariki siku ya Jumatatu. Alikuwa akisumbuliwa na Kisukari kwa muda mrefu na aliugua sana katika wiki za hivi karibuni. Khaled ameshazikwa katika kaburi la familia katika eneo la al-Basatin. Khitma yake ilifanyika katika Msikiti wa Al-Hamidiya al-Shazliya huko…
Mahesabu mabovu ya maadui kuhusu nguvu za irada na azma ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran walitumia uwezo na nguvu zao zote katika machafuko ya hivi karibu kujaribu kutoa pigo kwa Iran ya Kiislamu, lakini kama ilivyojiri kwa miaka ya huko nyuma, njama zao za mara hii pia zimesambaratika na kwa mara nyingine umoja na mshikamano wa wananchi pamoja na nguvu na uimara wa…