Vyombo vya Habari

Russia yatangaza kuwa tayari kutatua mgogoro wa Ukraine kwa njia ya mazungumzo

Russia yatangaza kuwa tayari kutatua mgogoro wa Ukraine kwa njia ya mazungumzo

Msemaji wa Ikulu ya Russia (Kremlin) ametangaza kuwa, nchi hiyo iko tayari kutatua mgogoro wa Ukraine kwa njia ya mazungumzo. Dmitry Peskov msemaji wa Ikulu ya Russia ameeleza kuwa, Moscow ipo tayari siku zote kutatua matatizo mbalimbali kwa njia ya mazungumzo; ambapo Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin mara kadhaa amebainisha juu ya azma ya…

Amnesty International: Marekani inapasa kufuta doa la Guantamano

Amnesty International: Marekani inapasa kufuta doa la Guantamano

Sambamba na maadhimisho ya kutimia mwaka wa 21 tangu kuanza kazi gereza la Guantanamo huko katika Ghuba ya Cuba; Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limelaani jinai za miaka 21 katika gereza hilo zilizotekelezwa na Wamarekani. Tarehe 11 Januari mwaka 2002 jela za kijeshi zilizokuwa chini ya ulinzi mkali sana katika kambi ya jeshi la…

UN: Marekani inahatarisha haki za binadamu kwa hatua zake mpakani

UN: Marekani inahatarisha haki za binadamu kwa hatua zake mpakani

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Volker Türk, ameonya kuwa mikakati mipya iliyotangazwa na serikali ya Marekani ya kudhibiti au kulinda mipaka yake inadumaza misinig ya kimataifa ya haki za binadamu. Taarifa iliyotolewa Jumtano jijini Geneva, Uswisi na ofisi ya kamishna huyo wa haki za  binadamu, OHCRC, imesema haki ya kusaka…

Msemaji wa Hamas: Utawala wa Kizayuni unafuatiliwa usiku na mchana

Msemaji wa Hamas: Utawala wa Kizayuni unafuatiliwa usiku na mchana

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameeleza kuwa mapambano ya kulinda na kuutetea msikiti wa al Aqsa na mateka wa Kipalestina yatakuwa ya aina yake na kusisitiza kuwa utawala wa Kizayuni unawajibika kubeba dhima ya matokeo ya hatua za kichochezi za Ben Gvir. Abdullatif al Qanui Msemaji wa Hamas amesema akihutubia…

Utawala wa Israel umeua wanahabari 55 wa Kipalestina tangu 2000

Utawala wa Israel umeua wanahabari 55 wa Kipalestina tangu 2000

Waandishi habari wapatao hamsini na watano wa Kipalestina wameuawa na utawala katili wa Israel tangu mwaka 2000 ikiwa ni katika njama za utawala huo wa kikoloni za kuzuia habari za jinai zake dhidi ya Wapalestina kuwafikia walimwengu. Waandishi hamsini na watano wameuawa, ima kwa kupigwa risasi au kwa kudondoshewa mabomu na Israel tangu mwaka 2000,”…

Qur’ani Tukufu yavunjiwa heshima katika hujuma dhidi Msikiti wa Sheffield, Uingereza

Qur’ani Tukufu yavunjiwa heshima katika hujuma dhidi Msikiti wa Sheffield, Uingereza

Baadhi ya nakala na Kurani Tukufu na vitabu vingine vya Kiislamu vilichanwa wakati wa shambulio la Msikiti wa Jamia Abdullah Bin Masood huko Sheffield, Uingereza. Shambulio hilo dhidi ya msikiti huo ulioko Sheffield, Yorkshire Kusini, linaashiria kuongezeka jinai za chuki dhidi ya Waislamu nchini Uingereza. Taarifa zinasema vifaa mbalimbali vya misikiti viliharibiwa na kuporwa na…

Uganda yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa Ebola ulioua makumi

Uganda yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa Ebola ulioua makumi

Uganda imetangaza habari ya kudhibitiwa na kutokomezwa mlipuko wa Ebola ambao umeua makumi ya watu nchini humo tangu Septemba mwaka uliomalizika 2022. Tangazo hilo limetolewa leo Jumatano na Jane Ruth Aceng, Waziri wa Afya wa Uganda katika hafla ya kuadhimisha mwisho wa mlipuko wa maradh hayo hatarishi. Dakta Aceng amebainisha kuwa, ‘Tumefanikiwa kudhibiti msambao wa Ebola…

Marekani yaongeza ulinzi kwa viongozi wa serikali ya Trump waliomuua Kamanda Soleimani

Marekani yaongeza ulinzi kwa viongozi wa serikali ya Trump waliomuua Kamanda Soleimani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kila mwezi inatumia zaidi ya dola milioni mbili kuwalinda saa 24 Mike Pompeo na Brian Hook, viongozi wa serikali ya Donald Trump waliohusika katika mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH. Kwa mujibu wa…