Fedheha! Uingereza yashindwa kutuma satalaiti yake anga za mbali
Jaribio la Uingereza la kuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kurusha satalaiti katika anga za mbali limegonga mwamba, huku kampuni ya Virgin Orbit ikitangaza kuwa roketi lake la kurushia satalaiti hiyo lilikubwa na hitilafu na kuifanya (satalaiti hiyo) ishindwe kufika katika anga za mbali. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, roketi la LauncherOne la…
Maelfu ya wauguzi wafanya mgomo New York, Marekani
Wauguzi zaidi ya 7,000 katika hospitali mbili kubwa jijini New York nchini Marekani wameanza mgomo baada ya mazungumzo yao na serikali kuhusiana na mazingira yao ya kazi, nyongeza ya mishara na sera za wafanyakazi kugonga mwamba. Chama cha Wauguzi Jimboni New York kimetangaza kuwa, mgomo huo katika hospitali mbili kuu za jiji hilo ulianza jana…
Biashara ya bidhaa za Iran yazidi kunawiri nchini Saudi Arabia
Usafirishaji nje wa bidhaa za Iran kuelekea nchini Saudi Arabia umestawi hivi sasa baada ya kuanza mazungumzo baina ya nchi hizi mbili za Waislamu. Hayo yametokea baada ya biashara baina ya pande mbili kuzorota kwa miaka kadhaa. Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Sayyid Rohollahi Latifi, mjumbe wa Kamati ya Kimataifa na Biashara…
Imarati yajikomba zaidi kwa Israel, shule za nchi hiyo kufunza ‘Holocaust’
Umoja wa Falme za Kiarabu unaendelea kujidhalilisha na kujipendekeza kwa utawala haramu wa Israel, na sasa shule za nchi hiyo zinazatamiwa kuanza kufundisha ‘ngano ya Holocaust’ yaani mauaji ya halaiki ya Wayahudi yanayodaiwa kufanywa na utawala wa Kinazi wa Ujerumani chini ya uongozi wa Adolf Hitler. Hayo yalitangazwa jana Jumatatu na ubalozi wa Imarati nchini…
Rabetu – Agizo la kuanzisha mahusiano mema ya kijamii – Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi (Mkuu wa shule Jamia Urwatul Wuthqa – Lahore) Imetolewa katika msikiti wa: Masjid Baitul ul Ateeq Lahore – Pakistan Januari 6, 2023 HOTUBA ya 1: Rabetu – Agizo la kuanzisha mahusiano mema ya kijamii Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu, na nawasisitizieni kuyasimamisha maisha yenu…
Kiongozi wa upinzani Kenya aonya kuhusu Msikiti kutumiwa katika malumbano ya kisiasa
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya amemuonya mwanasiasa maarufu Muislamu nchini humo kuhusu kuutumia Msikiti kama jukwaa la kisiasa. Kiongozi wa chama cha ODM na muungano wa upinzani wa Azimio Raila Odinga amemuonya Waziri wa Ulinzi Aden Duale dhidi ya kutumia Msikiti huo kama jukwaa la kisiasa. Akizungumza Ijumaa mjini Mombasa, Raila pia alimuonya Mwenyekiti…
Uganda yapeleka wanajeshi katika mpaka na DRC kuzuia waasi wa M23
Serikali ya Uganda imetangaza kuwa, imepeleka wanajeshi wake katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya kuwa tayari kukabiliana na waasi wa M23. Taarifa ya jeshi la Uganda UPF imeeleza kuwa, wanajeshi wake wamepelekwa katika wilaya ya Kanungu, ambako waasi wa M23 wameendelea kuingia katika mji wa Ishasha,…
China yaondoa vizuizi vyote vya Covid-19 kwa wasafiri
Serikali ya China imetangaza kufungua tena mipaka yake kwa wageni wa kimataifa kwa mara ya kwanza tangu ilipoweka vizuizi vya kusafiri mnamo Machi 2020 kufuatia janga la corona. Wasafiri wanaoingia hawatahitaji tena kuwekewa karantini hatua ambayo inaashiria mabadiliko makubwa katika sera ya serikali ya Beijing ya Covid-19. Tangazo hilo linatolewa katika hali ambayo, kwa sasa China…