Russia yaua askari 600 wa Ukraine katika shambulio la kulipiza kisasi
Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa, wanajeshi 600 wa Ukraine wameangamizwa katika shambulio la makombora la ulipizaji kisasi la Moscow katika eneo la Donbass. Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa, shambulio hilo la jana Jumapili la makombora katika mji unaoshikiliwa na Kiev wa Kramatorsk katika eneo la Donbass ilikuwa ‘operesheni ya kulipiza kisasi’ dhidi ya jeshi…
Polisi Ufaransa yashambulia waandamanaji wa ‘Vizibao vya Njano’
Askari polisi nchini Ufaransa wamewashambulia vibaya maelfu ya watu walioshiriki maandamano ya Vizibao vya Njano, kulalamikia sera za Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo na hususan mageuzi tata ya pensheni yanayotazamiwa kuanza kutekelezwa mwaka huu wa 2023. Polisi ya Ufaransa imewashambulia waandamanaji hao waliokuwa wamekusanyika katika medani ya Breteuil mjini Paris kwa mabomu ya gesi ya…
Maelfu ya wakimbizi wa Rohingya waendelea kutangatanga hawajui pa kwenda
Boti yenye wakimbizi Waislamu 185 wa Rohingya imewasili katika jimbo la Aceh, nchini Indonesia. Mamia ya wakimbizi waliwasili mwaka uliopita kutokana na hali mbaya katika kambi za wakimbizi nchini Bangladesh. Zaidi ya nusu ya wakimbizi hao waliowasili jana mchana nchini Indonesia, ni wanawake na watoto. Wengi wao wameonekana wakiwa wamelala kwenye mchanga kutokana na uchovu…
UNICEF: Watoto wapatao milioni 4 Pakistani wangali wanaishi kwenye maji machafu
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetangaza kuwa, watoto wapatao milioni 4 nchini Pakistan wangali wanaishi kwenye maji machafuko yaliyosimama. Taarifa ya UNICEF imebainisha kuwa, zaidi ya miezi minne tangu kutangazwa kwa hali ya dharura, zaidi ya watoto milioni 4 bado wanaishi karibu au kwenye maji ya mafuriko yaliyosimama na hivyo kutishia uhai…
Kuendelea kukandamizwa wanawake nchini Saudi Arabia
Wanaharakati 35 wa kike wa Saudi Arabia wamehukumiwa kifungo cha miaka 11 jela ikiwa ni muendelezo wa ukandamizaji unaofanywa na ukoo wa Aal Saud dhidi ya wanawake. Saudi Arabia ni miongoni mwa nchi zenye historia mbaya sana ya uvunjaji wa haki za wanawake duniani. Takwimu zinaonesha kuwa, utulivu na usalama kwa wanawake wa Saudia ulikuwa…
Mazungumzo ya Mawaziri wa Ulinzi wa Imarati na Syria mjini Damascus yaikasirisha Washington
Washington imetoa radiamali kufuatia ziara ya karibuni ya Waziri wa Ulinzi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) mjini Damascus na kutishia kuwa, hatua yoyote ya Imarati kuhuisha uhusiano na serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria itazigharimu pande mbili hizo. Abdullah bin Zayed Al Nahyan Waziri wa Ulinzi wa Imarati hivi karibuni alifanya…
Sheikh Naim Qassim: Hujuma za kihabari na kigaidi za Marekani dhidi ya Iran zimegonga mwamba
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, hujuma za kihabari na kigaidi za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zilizokuwa zikiendeshwa katika fremu ya machafuko yaliyokuwa yameibuka nchini Iran zimesambaratika na kugonga mwamba. Samahat Sheikh Naim Qassim, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu…
AFRICA CDC: Mlipuko wa Ebola Uganda umedhibitiwa, unakaribia kumalizika
Mlipuko wa Ebola nchini Uganda umedhibitiwa na unaweza kutangazwa kuwa umekwisha katika siku chache zijazo, kwani zimepita siku 39 tangu kisa cha mwisho cha virusi hivyo kuripotiwa. Hayo ni kwa mujibu wa tangazo la Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (AFRICA CDC). Ahmed Ogwell Ouma, kaimu mkuu wa AFRICA CDC amesema hadi kufikia…