Genge la kigaidi la al Shabab laomba mazungumzo na serikali
Serikali ya Somalia ilitangaza jana Jumamosi kwamba genge la kigaidi na ukufurishaji la al Shabab limeomba kufanya mazungumzo na serikali hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa genge hilo kuomba kukutana na kuzungumzo na serikali ya Mogadishu. Ombi hilo la al Shabab limekuja huku vikosi vya serikali vikiendelea kupambana na genge hilo kigaidi ambalo limetangaza…
Kipindupindu chazidi kuitesa Malawi; Tanzania yakaa chonjo
Visa vya maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kipindupindu nchini Malawi vimezidi kuongezeka huku mikoa ya Tanzania inayopakana na nchi hiyo mikakati ikizidi kuimarishwa ili ugonjwa huo usiingie. Taarifa zaidi zinasema kuwa, idadi ya watu wanaopoteza maisha kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Malawi imezidi kuongezeka kutoka watu 661 hadi kufikia vifo 687. Akizungumza na…
Ongezeko la maneno ya kibaguzi dhidi ya Waafrika katika Twitter
Ongezeko la matumizi ya maneno ya kibaguzi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika kwenye mtandao wa Twitter kufuatia umiliki mpya wa kampuni hiyo ni jambo ambalo limeibua hoja ya kuzitaka kampuni za mitandao ya kijamii kuwajibika zaidi kuhusu chuki inayoelekezwa dhidi ya watu hao. Hayo yamesemwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki…
Rais wa Mauritania atembelea maonesho ya Qur’ani Tukufu mjini Nouakchott
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani ametembelea maonyesho ya Qur’ani Tukufu katika mji mkuu wa nchi hiyo Nouakchott. Hafla hiyo ya Qur’ani kwa wanaume na wanawake itaendeshwa katika maeneo tofauti huko Dubai kwa siku tano. Kwa mujibu wa Ibrahim Mohamed Bu Melha, mshauri wa Mtawala wa Dubai kwa Masuala ya Utamaduni na Kibinadamu na mwenyekiti…
Kufichuliwa jinai za Uingereza nchini Afghanistan
Mwanamfalme Harry wa ukoo wa kisultani na kifalme wa Uingereza amekiri kuua watu 25 nchini Afghanistan wakati wa vita vya miaka mingi vya nchi hiyo. Harry ambaye ni maarufu kwa jina la Duke of Sussex, ni mtoto mdogo wa Charles III, mfalme wa hivi sasa wa Uingereza. Hivi karibuni Harry alitanga kujitoa kwenye ukoo wa kifalme…
“Walimwengu wamekuwa watazamaji tu wa jinai za Saudia dhidi ya Wayamen”
Kituo cha Haki za Binadamu cha Yemen cha Ainu Yemen (Jicho la Yemen) kimetoa radiamali yake kuhusiana na jinai mpya za muungano vamizi unaoongozwa na utawala wa Saudi Arabia na kutangaza kuwa, jamii ya kimataifa imeamua kuwa mtazamaji tu wa jinai zinazofanywa na Aal Saud na washirika wake huko nchini Yemen. Kituo hicho sambamba na…
Kongamano la kitaaluma la maulamaa wa Ulimwengu wa Kiislamu lafanyika Tanzania
Kongamano la kitaaluma la wanazuoni wa Ulimwengu wa Kiislamu limefanyika jijini Dar es Salaam kwa kuhudhuriwa na wanafikra kutoka Tanzania na Iran. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB katika kongamano hilo wahadhiri wa vyuo vikuu na watafiti waliwasilisha makala zenye anuani “umuhimu wa maelewano kati ya wanazuoni wa Ulimwengu wa…
Rais wa Mauritania asifu misimamo thabiti ya Iran kwa masuala ya Ulimwengu wa Kiislamu
Rais Mohamed Ould Ghazouani wa Mauritania amepongeza misimamo thabiti na ya kimsingi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na masuala ya Ulimwengu wa Kiislamu. Ould Ghazouani ametoa pongezi hizo katika mazungumzo na Mohammad Mehdi Esmaili, Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Iran. Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Iran, yuko Nouakchott,…