Russia yalalamikia vikao visivyoisha vya UN kuhusu faili la silaha za kemikali la Syria
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amelalamikia vikao visivyoisha na vya kila mwezi vya Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu faili la silaha za kemikali la Syria na kusema kuwa, vikao hivyo vinafanyika kiudanganyifu kwa manufaa ya baadhi ya nchi za Magharibi. Shirika la habari la IRNA limemnukuu Dmitry Polyanskiy akisema…
Taliban: Mauaji aliyofanya mwanamfalme wa Uingereza Afghanistan ni “uhalifu wa kivita”
Kufuatia kauli ya mwanamfalme wa Uingereza Harry, ya kuungama kwamba aliua Waafghani 25 wakati wa vita nchini Afghanistan, maafisa wa serikali ya Taliban wametangaza kuwa hatua hiyo ya mwanamfalme huyo wa Uingereza ni uhalifu wa kivita. Anas Haqqani, mwanachama mwandamizi wa Taliban, ameeleza katika ujumbe wa Twitter aliotuma kujibu matamshi ya mwanamfalme Harry wa familia ya…
Mtoto wa miaka 6 ampiga risasi mwalimu wake kwa ‘makusudi’ Marekani
Mtoto wa miaka sita huko nchini Marekani ametiwa mbaroni baada ya kumpiga risasi na kumjeruhi vibaya mwalimu wake katika mji wa Newport News, jimboni Virginia. Mkuu wa Polisi katika mji wa Newport News, Steve Drew amethibitisha habari ya kutokea tukio hilo hapo jana Ijumaa katika shule ya msingi ya Richneck, katika mji wa Newport News, jimboni Virginia, kusini…
‘Uhuru wa kujieleza’, kisingizio cha kukaririwa cha Charlie Hebdo kwa ajili ya kutusi matukufu wa kidini
Jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo, ambalo huko nyuma lilidhalilisha na kumvunjia heshima mara kadhaa Mtume Mtukufu wa Uislamu (saw), sasa limeimarisha chuki zake dhidi ya dini hii tukufu kwa kutukana na kuwavunjia heshima viongozi wa kidini na kisiasa wa Kiislamu. Jarida la dhihaka la Charlie Hebdo hivi karibuni liliandaa shindano la kimataifa la uchoraji…
Wasiwasi wa kieneo na kimataifa kuhusu tabia ya ubaguzi wa rangi ya baraza jipya la mawaziri la Israel dhidi ya Wapalestina
Hatua ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa utawala haramu wa Israel, ya kuingia kinyume cha sheria katika Msikiti Mtukufu wa al-Aqsa imekabiliwa na radiamali kali ya kieneo na kimataifa, na ambayo imezipelekea nchi za China na Imarati kuomba kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili…
Wayemen waandamana kitaifa dhidi ya muungano vamizi wa Saudia-Marekani
Jana Ijumaa, wananchi wa Yemen walifanya maandamano makubwa katika mikoa mbalimbali kulaani uvamizi wa muungano wa Saudia na Marekani dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu na kuendelea kuzingirwa kila upande nchi yao pamoja na vitendo mbalimbali vya kuchochea vita vinavyofanya na madola vamizi. Kwa mujibu wa televisheni ya al Alam, mamia ya maelfu ya wananchi…
Umoja wa Mataifa wampongeza Samia kwa kuruhusu mikutano ya hadhara ya kisiasa
Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu (OHCHR) imepongeza hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutangaza kuondoa marufuku kwa vyama vya siasa nchini humo kufanya mikutano ya hadhara. Msemaji wa ofisi hiyo kutoka Nairobi, Kenya Seif Magango amesema kuwa, “hatua hii ambayo ameichukua…
WHO: Tunatumai 2023 utakuwa mwisho wa janga la dunia nzima la Covid-19
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema, kuna matumaini kwamba janga la dunia nzima la ugonjwa wa Covid-19 litamalizika katika mwaka huu wa 2023. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni katika jedwali la dunia nzima la Corona, Marekani ndiyo inayoongoza kimaafa kwa kuwa na watu milioni 102,963,370 walioambukizwa virusi vya corona na…