Kurudi nyuma kwa serikali ya Macron dhidi ya upinzani
Serikali ya Ufaransa Jumanne wiki hii ilidokeza uwezekano wa kutazamwa umpya mpango tata wa Rais Emmanuel Macron wa kubadilisha sheria za pensheni. Hatua hiyo inaonekana kuwa ni kusalimu amri mbele ya wapinzani wa mpango huo. Waziri Mkuu wa Ufaransa, Élisabeth Borne amesema kabla ya mazungumzo na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi, ambao wanapinga vikali mabadiliko…
Indhari baada ya kuongezeka joto, katikati ya msimu wa baridi barani Ulaya
Mamia ya vituo vya hali ya hewa kote Ulaya vimerekodi viwango vya juu vya joto kila siku kuwahi kufikiwa katika miezi ya Desemba au Januari. Huduma kadhaa za kitaifa za hali ya hewa na maji kutoka bara hilo zinathibitisha kuwa mwaka wa 2022 ulikuwa wa joto zaidi katika historia katika nchi hizo. Hayo ni kwa…
Baraza la Usalama la UN lashindwa kuchukua hatua baada ya waziri wa Israel kuvamia al-Aqsa
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamesisitiza ulazima wa kudumisha hali ya miongo kadhaa iliyopita katika eneo la Msikiti wa al-Aqsa katika Mji Mkongwe wa al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel baada ya waziri mmoja wa Israel kulivunjia heshima eneo hilo takatifu. Tamko hilo la Baraza la Usalama limekuja kwa kuchelewa…
Kuongezeka umaarufu wa Shahidi Haj Qassem Soleimani duniani, hasa barani Asia
Sambamba na kuadhimishwa mwaka wa tatu wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Haj Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandes, habari na ripoti zilizochapishwa kuhusu kufanyika sherehe katika maeneo mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa uungwaji mkono na umaarufu wa jenerali huyo mashuhuri umeongezeka zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma, na hasa miongoni mwa vijana. Katika uwanja huo, mipango na…
Marekani ilikiuka mamlaka ya kujitawala Iraq kwa kuwaua Jenerali Soleimani na Al Muhandis
Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia’ al-Sudani amemuenzi kamanda wa ngazi ya juu wa kupambana na ugaidi wa Iran, Luteni Jenerali Qassem Soleimani na mwenzake wa Iraq, Abu Mahdi al-Muhandis, waliouawa katika shambulio la kigaidi la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad miaka mitatu iliyopita, na kusema kuwa…
Rdiamali ya Waziri wa Utamaduni wa Iran kwa hatua ya udhalilishaji ya jarida la Kifaransa
Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran ametoa radiamali yake kupitia ukurasa wake wa kijamii kuhusu hatua ya dharau na udhalilishaji iliyochukuliwa karibuni na jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo dhidi ya Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Katika toleo lake maalumu la siku ya Jumatano tarehe 4 Januari, jarida hilo…
Majambazi wateka nyara watu 63 nchini Nigeria baada ya kushambulia maficho yao
Watu wenye silaha, ambao wenyeji wanaamini ni majambazi wameteka nyara makumi ya wakazi wa Jimbo la Niger nchini Nigeria baada ya vikosi vya usalama kuokoa watu wengine 13. Ingawa msemaji wa polisi, Wasiu Abiodun, amekataa kuthibitisha ni watu wangapi hasa waliotekwa nyara katika jamii tatu za jimbo hilo la Niger, lakini baadhi ya duru za usalama zimefichua…
Onyo la Bunge la Misri kuhusu njaa na ughali wa bidhaa muhimu
Wabunge wa Misri, wameonya kuhusu njaa na ughali wa bidhaa nchini humo na kusisitiza kuwa Wamisri wamechoshwa na hali hiyo. Wameituhumu serikali kuwa imeshindwa kabisa kukabiliana na mfumuko wa bei uliokithiri nchini kuhusu bidhaa za msingi. Sambamba na kuanza mwaka huu mpya wa 2023, bei ya jbidhaa za msingi imeongezeka maradufu katika masoyo ya Misri…