Putin atuma manowari yenye makombora ya hypersonic Bahari ya Atlantic, Hindi
Rais Vladimir Putin wa Russia ameagiza kutumwa katika Bahari ya Atlantic na Bahari Hindi meli ya kivita iliyosheheni makombora ya hypersonic huku vita vya Ukraine vikipamba moto. Rais Putin jana Jumatano kupitia njia ya video, alishiriki katika hafla ya kuiaga manowari hiyo ya kijeshi ya ‘Admeli Gorshkov’ kuelekea Bahari ya Atlantic na Bahari Hindi. Sergei Shoigu, Waziri wa Ulinzi…
Bei za bidhaa UK zavunja rekodi ya miaka 20; vita Ukraine moja ya sababu
Utafiti wa karibuni kabisa unaonesha kuwa, bei za bidhaa muhimu zimepaa vibaya nchni Uingereza na kuvunja rekodi ya miongo miwili iliyopita, suala ambalo limepandisha mno ughali wa maisha. Wataalamu wa mambo wanasema, vita vya Ukraine na kitendo cha nchi za Magharibi cha kuiwekea vikwazo Russia kimechangia sana katika hali hiyo mbaya ya maisha huko Uingereza….
Kuendelea mwenendo wa kufutwa kazi wafanyakazi huko Marekani; Amazon kupunguza wafanyakazi elfu 18
Mkurugenzi Mtendaji wa Amazon amesema kuwa kampuni hiyo itawafuta kazi wafanyakazi zaidi ya 18,000. Baadhi ya waajiri wakubwa wa Marekani, ikiwa ni pamoja na Walmart, Facebook na Pepsi, hivi karibuni wamepunguza maelfu ya nafasi za kazi nchini humo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Andy Jaycee amesema leo Alhamisi kwamba idara muhimu zitakazopunguziwa…
Asilimia 70 ya Wamarekani wana wasiwasi wa kutokea vita vya nyuklia
Uchunguzi wa hivi karibuni wa maoni unaonesha kuwa asilimia 70 ya wananchi wa Marekani wana wasiwasi wa kutokea vita vya nyuklia. Kuendelea vita nchini Ukraine na vikwazo dhidi ya Moscow sambamba na kuendelea nchi za Magharibi kuirundikia silaha Ukraine ni sababu ya wasiwasi huo wa asilimia kubwa ya Wamarekani kuhusu kutokea vita vya atomiki duniani….
Hisia na misimamo ya nchi za Kiarabu kwa uamuzi wa serikali ya Netanyahu wa kupanua vitongoji haramu vya wazayuni
Kufuatia uamuzi uliotangazwa na waziri mkuu mpya wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba serikali yake itaendeleza ujenzi haramu wa vitongoji, baadhi ya nchi za Kiarabu zimelaani uamuzi huo na kuipa indhari Tel Aviv kuhusiana na madhara ya hatua hiyo. Katika kikao cha bunge la utawala haramu wa Israel cha kulipigia baraza…
HAMAS: Viongozi wa nchi za Kiislamu amkeni kukiokoa Kibla cha Kwanza
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amewatahadharisha viongozi wa nchi za Kiislamu kuhusuu njama za kila namna za serikali mpya ya kifashisti ya Israel na kuwataka waamke kukiokoa Kibla cha Kwanza cha Waislamu. Mashirika ya habari ya yamemnukuu Ismail Hania akitoa tahadhari hiyo jana (Jumatano) na kuzitaka nchi…
Umoja wa Ulaya washindwa kulaani uchochezi wa waziri mwenye itikadi za kibaguzi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa.
Kitendo cha uchochezi cha waziri mwenye itikadi kali na za kibaguzi wa baraza la mawaziri la utawala haramu wa Israel katika kuuvunjia heshima Msikiti wa al-Aqsa hakijakabiliwa na hatua yoyote ya maana kutoka kwa Umoja wa Ulaya. Itamar Ben-Gvir, waziri wa usalama wa ndani wa utawala wa Kizayuni aliingia katika Msikiti wa al-Aqsa Jumanne iliyopita…
Kutimuliwa balozi wa Ufaransa Burkina Faso; pigo jengine kwa Paris
Msemaji wa serikali ya Burkina Faso Jean-Emmanuel Ouedraogo ametangaza kuwa balozi wa Ufaransa Luc Hallade ametakiwa aondoke nchini humo kufuatia kushadidi mgogoro kati ya nchi hizo mbili. Ufaransa na Burkina Faso zimekuwa zikizozana tangu yalipotokea mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso Septemba 30 mwaka uliopita yaliyoongozwa na Ibrahim Traoré, kapteni wa jeshi mwenye umri wa…