Vyombo vya Habari

Milipuko miwili ya mabomu ya kutegwa garini yauwa watu tisa katikati mwa Somalia

Milipuko miwili ya mabomu ya kutegwa garini yauwa watu tisa katikati mwa Somalia

Milipuko miwili ya mabomu imeuwa raia wasiopungua tisa na kujeruhi wengine kadhaa katikati ya Somalia. Abdullah Adam afisa usalama wa Somalia amesema kuwa  watu wasiopungua 9 wameuawa na wengine 15 wamejeruhiwa katika milipuko miwili ya mabomu ya kutegwa ndani ya gari iliyotokea kwa wakati mmoja mapema leo Jumatano katika mji wa Mahas kwenye mkoa wa…

Wafanyakazi wa reli nchini Uingereza kuanza mwaka mpya na mgomo

Wafanyakazi wa reli nchini Uingereza kuanza mwaka mpya na mgomo

Abiria wa reli ya Uingereza wametahadharishwa kuhusu kutatizika safari mwanzoni mwa mwaka mpya, huku wafanyakazi wa reli wakianzisha mgomo wa kwanza jana. Uingereza sasa iko katika hali mbaya zaidi ya migomo ya wafanyikazi tangu Margaret Thatcher aingie madarakani miaka ya 1980, huku mfumuko wa bei ukifuatia zaidi ya miaka 10 ya ukuaji wa mishahara uliodorora,…

Bunge la Marekani lashindwa kumpata Spika; McCarthy ang’ang’ania licha ya kuangushwa mara tatu

Bunge la Marekani lashindwa kumpata Spika; McCarthy ang’ang’ania licha ya kuangushwa mara tatu

Baraza la Wawakilishi nchini Marekani jana lilishindwa kumpata Spika mpya wa Bunge la nchi hiyo licha ya uchaguzi huo kufanyika mara tatu. Baada ya duru tatu za upigaji kura, Bunge liliahirisha mchakato huo hadi saa sita mchana leo Jumatano. Ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 100 ambapo hakuna Mrepublikan au Mdemokrat aliyeshinda uspika…

Ayatullah Sistani ahimiza uungwaji mkono kwa Afghanistan

Ayatullah Sistani ahimiza uungwaji mkono kwa Afghanistan

Kiongozi mkuu wa Waislamu wa Kishia nchini Iraq Ayatullah Seyed Ali al-Sistani amehimiza jumuiya ya kimataifa na Waislamu kote ulimwenguni kuunga mkono watu “wanaoteseka” nchini Afghanistan. Aliyasema hayo katika mkutano wa Jumanne katika ofisi yake yenye makao yake makuu mjini Najaf akiwa na ujumbe i wa Baraza la Ulamaa wa Kishia la Afghanistan. Akirejelea uhalifu…

Wananchi Marekani hawamtaki Biden wala Trump kugombea tena katika uchaguzi 2024

Wananchi Marekani hawamtaki Biden wala Trump kugombea tena katika uchaguzi 2024

Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa hivi karibuni huko Marekani yanaonyesha kuwa akthari ya wapiga kura wa nchi hiyo wanapinga Joe Biden na Donald Trump, rais wa sasa na wa kabla yake, kugombea tena katika uchaguzi wa rais mwaka 2024. Uchaguzi ujao wa rais wa Marekani umepangwa kufanyika tarehe 5 Novemba mwaka 2024. Shirika…

Chuo cha al-Azhar chalaani waziri Mzayuni kuvamia msikiti mtakatifu wa al-Aqswa

Chuo cha al-Azhar chalaani waziri Mzayuni kuvamia msikiti mtakatifu wa al-Aqswa

Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar cha nchini Misri kimelaani vikali hatua ya waziri Mzayuni mwenye misimamo ya kufurutu ada kuvamia msikiti wa mtakatifu wa al-Aqswa, kibla cha kwanza cha Waislamu. Taarifa ya Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri imeeleza kuwa, hatua ya waziri huyo ni ya kichochezi na inaonyesha kuingiwa na woga na wahaka…

Burkina Faso yamtimua balozi wa Ufaransa nchini humo

Burkina Faso yamtimua balozi wa Ufaransa nchini humo

Serikali ya Burkina Faso imetangaza kwamba imemtaka balozi wa Ufaransa mjini Ouagadougou, Luc Hallade, aondoka nchini humo. Hatua hiyo imechukuliwa katika kivumbi cha mvutano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili. Kufukuzwa kwa balozi Luc Hallade wa Ufaransa kumefanyika wiki mbili baada ya Barbara Manzi, mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kibinadamu nchini Burkina…

Rais Samia: Mikutano ya hadhara ya kisiasa sasa ruhsa Tanzania

Rais Samia: Mikutano ya hadhara ya kisiasa sasa ruhsa Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania leo Jumanne, Januari 3, 2022 amekutana na viongozi wa vyama 19 venye usajili kamili wa siasa nchini humo Ikulu jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa, ni haki kwa vyama vya siasa kuendesha mikutano yao ya hadhara nchini humo lakini kuna wajibu wa kila mmoja na upande wa Serikali…