Zakzaky: Ni wajibu kwa Waislamu wote huru kuendeleza njia ya shahidi Soleimani
Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesisitiza kuwa, vijana wa kambi ya muqawama wanapaswa kusimama imara kukabiliana na madola ya kiistikbari kama ambavyo pia amewataka Waislamu kutumia njia zote zinazowezekana, kuhakikisha fikra za shahidi Qassem Soleimani zinabakia hai. Sheikh Ibrahim Zakzaky amesema hayo katika mahojiano na shirika la habari la FARS kwa mnasaba wa…
Sweden yafunga shule kadhaa za Kiislamu kwa visingizio mbalimbali
Jumuiya ya shule za Kiislamu nchini Sweden imetangaza kufungwa baadhi ya shule za Kiislamu ambazo baadhi yao ziliasisiwa katika muongo wa 90. Katika miaka ya karibuni baadhi ya nchi za Ulaya na makundi yenye misimamo mikali yamekuwa yakihujumu Uislamu na matukufu yake katika fremu ya propaganda chafu za kuchafua sura halisi ya dini hiyo na wafuasi wake. Serikali…
Makumi ya Wamarekani, wahanga wa umaskini na baridi kali, huku mabilioni ya dola yakitumiwa kwenye vita vya Ukraine
Wakati mji wa Buffalo ulioko katika jimbo la New York kaskazini-mashariki mwa Marekani, ukihangaika kujikwamua kwenye athari mbaya za theluji na dhoruba kali, matatizo yaliyosababishwa na maafa hayo makubwa yamedhihirisha zaidi ukosefu wa usawa wa kiuchumi na ubaguzi wa kimbari katika mji huo na Marekani kwa ujumla. Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, kukata tamaa…
Nyumba 200 zateketezwa kwa moto nchini Afrika Kusini
Moto mkubwa uliotokea katika kitongoji duni nje kidogo ya mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini umeua mwanamke mmoja na kuharibu zaidi ya nyumba 200. Tukio hilo la moto lilitukia mapema usiku wa kuamkia jana Jumatatu katika eneo la makazi duni la Philippi viungani mwa Cape Town. msemaji wa shirika la misaada ya kibinadamu la Gift…
Trump atalipa gharama kubwa kwa mauaji ya Soleimani na Muhandis: Makundi ya mapambano ya Iraq
Kiongozi wa kundi la mapambano la Asa’ib Ahl al-Haq la nchini Iraq amesema rais wa zamani wa Marekani Donald Trump atalipa gharama kubwa kwa kuhusika na mauaji ya kigaidi dhidi ya mashujaa wawili wa mapambano dhidi ya ugaidi, Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis. Qais al-Khazali aliyasema hayo hivi karibuni katika hafla ya kuwakumbuka…
Malawi yaahirisha kufunguliwa kwa shule kutokana na visa vya kipindupindu
Malawi siku ya Jumatatu imeahirisha kufunguliwa kwa shule za msingi na sekondari kwa angalau wiki mbili kutokana na mlipuko wa kipindupindu. Muhula huo mpya ulipangwa kuanza Januari 3, lakini ongezeko la visa vya maambukizi ya kipindupindu na vifo vimeilazimu serikali kufuta mipango ya kufungua shule inapokabiliana na mlipuko huo. Hatua hiyo, kulingana na serikali, inahusu…
9 wafariki, wakiwemo watoto 6 katika msongamano wa mkesha wa mwaka mpya Uganda
Watu wasiopungua tisa wamefariki dunia wakiwemo vijana wadogo sita katika msongamano uliotokea wakati wa sherehe za mkesha wa mwaka mpya katika duka kuu moja la mji mkuu wa Uganda, Kampala. Kwa mujibu wa msemaji msaidizi wa polisi ya Uganda Luke Owoyesigyire, inasemekana tukio hilo lilitokea usiku wa manane wa kuamkia jana katika duka kuu la Freedom…
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu: Suala la maendeleo ya kisayansi na kuvuka mipaka ya elimu halipasi kusahaulika
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika mazungumzo na wawakilishi wa Baraza Kuu la Muungano wa Jumuiya za Wanachuo wa Kiislamu barani Ulaya kuwa suala la maendeleo ya kisayansi na kuvuka mipaka ya elimu halipasi kusahaulika. Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema leo Jumanne alipoonana na wawakilishi wa Baraza Kuu la…