Vitisho vya ajabu vya Marekani kwa Russia; ukiacha kutuuzia mafuta tutakuadhibu
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, White House mapema leo Jumanne ametoa vitisho vya ajabu dhidi ya Moscow baada ya nchi za Magharibi kuainisha bei maalumu ya kununulia mafuta ya Russia, na kusema kuwa hakushangazwa na radiamali iliyooneshwa na Kremlin. Shirika la habari la FARS limemnukuu Karine Jean-Pierre akisema hayo mapema leo na kuongeza kuwa, iwapo Russia…
Kukiri Marekani na Israel kuhusu kutotetereshwa Iran na machafuko ya hivi karibuni
Sambamba na himaya na uungaji mkono wa Marekani kwa wafanya fujo na machafuko nchini Iran, wachambuzi waandamizi wa masuala ya usalama wa Marekani na utawala haramu wa Israel wamekiri kwamba, Iran haijatetereshwa na machafuko hayo ya hivi karibuni. Avril Haines, Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa wa Marekani sanjari na kuashiria vurugu na machafuko ya Iran…
Wapalestina 160 wameuawa shahidi tangu kuanza mwaka huu
Kwa akali Wapalestina 160 wameuawa shahidi na jeshi la utawala haramu wa Israel katika ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan tangu kuanza mwaka huu wa 2022. Sambamba na mauaji hayo, wanajeshi wa Israel wakishirikiana na walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakifanya hujuma katika maeneo mbalimbali ya Wapalestina kwa ajili ya kusukuma mbele mpango mchafu wa kujitanua…
Jenerali Bagheri: Adui ameanzisha ‘Vita vya Utambuzi na Vyombo vya Habari’ kukabiliana na Iran
Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kupoteza matumaini adui katika medani ya kukabiliana ana kwa ana na Iran kijeshi na kusema: “Ni kwa sababu hii ndio adui ameanzisha vitisho katika mitandao ya intaneti, vita vya utambuzi na vita vya vyombo vya habari dhidi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.”…
Hungary yasamehewa kununua nishati ya Russia, yazionya nchi nyingine za Ulaya
Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kiuchumi wa Hungary amezionya nchi nyingine za Ulaya kwa uamuzi wao wa kuweka kiwango maalumu cha bei ya kununulia mafuta ya Russia na kusisitiza kuwa, uamuzi huo utatoa pigo kubwa zaidi kwa uchumi wa nchi za bara hilo. Péter Szijjártó amesema hayo kwenye mtandao wa kijamii wa…
National Interest: Vita vya pili vya ndani vimeanza nchini Marekani
Tovuti ya jarida la Marekani la National Interest limegusia vitendo vya kikatili vilivyofanywa na magaidi wa ndani ya Marekani na kusema kuwa, vita vya pili vya ndani vimeanza katika nchi hiyo ya Magharibi. Katika ripoti yake ya jana (Jumapili), shirika la habari la IRNA limelinukuu jarida hilo la Marekani likisema kuwa, watu waliofanya machafuko walikabiliana…
Wasiwasi kuhusu hasara za Ulaya katika vita vya Ukraine
Baada ya kupita takriban miezi 10 tangu kuanza vita vya Ukraine na thari zake mbaya, mkuu wa Baraza la Ulaya amekiri kwamba, nchi za bara hilo zimepata hasara zaidi katika vita hivyo kuliko Marekani. Licha ya kukiri kwamba vita vya Ukraine vimeziathiri Ulaya na Marekani kwa njia tofauti na kwamba Ulaya imepata hasara zaidi, mkuu…
Vitisho vya kukandamizwa waandamanaji nchini Uingereza
Katika miezi michache iliyopita, matatizo ya kiuchumi na kijamii katika nchi za Ulaya, hasa Uingereza, yameongezeka na kusababisha maandamano ya kijamii na mikusanyiko katika nchi hizo. Mikusanyiko mingi imekabiliwa na ukandamizaji wa vikosi vya polisi ambavyo vimekuwa vikitumia mkono wa chuma kuwatawanya waandamanaji. Kuhusiana na suala hilo, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ametetea utendaji…