Vyombo vya Habari

Yemen: Tunao uwezo wa kujibu shambulio lolote kwa makombora na droni

Yemen: Tunao uwezo wa kujibu shambulio lolote kwa makombora na droni

Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vinao uwezo wa kujibu mapigo dhidi ya shambulio lolote lile. Brigedia Saree ameeleza katika taarifa: “huko nyuma, maadui walikuwa wakishambulia Sana’a na mikoa mingine kwa mabomu na makombora bila kujibiwa; lakini leo tunao uwezo wa kujibu shambulio lolote lile kwa…

Walio hatarini kunyongwa Saudia kwa sababu za kiitikadi wafikia 59

Walio hatarini kunyongwa Saudia kwa sababu za kiitikadi wafikia 59

Vyombo vya mahakama vya Saudi Arabia vimepitisha hukumu ya adhabu ya kifo kwa vijana kadhaa waliowekwa kizuizini ukiwa ni mwendelezo wa utoaji hukumu za kifo kiholela kwa raia wanaoshikiliwa kwa sababu za kiitikadi. Faili la haki za binadamu la Saudi Arabia limetapakaa damu za watu wasio na hatia hususan Waislamu wa madhehebu ya Shia wa nchi hiyo,…

Viongozi wa kidini wakutana mashariki mwa Kongo kujadili hali ya mambo

Viongozi wa kidini wakutana mashariki mwa Kongo kujadili hali ya mambo

Viongozi wa kidini wamekutana katika mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia machafuko yaliyosababisha vifo vya watu 50 mashariki mwa nchi hiyo. Itakumbukwa kuwa, Alhamisi iliyopita jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lililituhumu kundi la waasi la M23 kwa mauaji hayo na kukiuka mapatano ya kusitisha vita yaliyofikiwa hivi karibuni. Mchungaji Samuel…

Ulyanov: Ulaya ifikirie kuishi bila ya mafuta ya Russia

Ulyanov: Ulaya ifikirie kuishi bila ya mafuta ya Russia

Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika taasisi za kimataifa mjini Vienna, Austria amesema kuwa, kuanzia mwaka ujao Ulaya itaishi bila ya mafuta ya Russia kufuatia hatua yake ya kuainisha bei ya mafuta kutoka Russia. Mikhail Ulyanov ametoa matamshi hayo akijibu hatua ya nchi za Magharibi na Umoja wa Ulaya ya kuianisha bei ya dola 60…

Sheria ya Bunge: Wazinifu nchini Indonesia kufungwa jela

Sheria ya Bunge: Wazinifu nchini Indonesia kufungwa jela

Bunge la Indonesia limo mbioni kupasisha sheria ya kutoa adhabu kwa wanaofanya zinaa nchini humo, hatua ambayo inalenga kukabiliana na vitendo vya uasherati. Taarifa kutoka Indonesia zinasema, Bunge la nchi hiyo linatarajiwa kupitisha sheria ya uhalifu mwezi huu itakayowaadhibu watu wanaoshiriki ngono nje ya ndoa na kwamba, adhabu hiyo inaweza kufikia kifungo cha hadi mwaka…

Indonesia yakataa kumpokea mjumbe maalumu wa kutetea ubaradhuli wa Marekani

Indonesia yakataa kumpokea mjumbe maalumu wa kutetea ubaradhuli wa Marekani

Marekani imelazimika kufuta safari ya mjumbe wake maalumu wa kutetea eti haki za mabaradhuli (LGBTQ) nchini Indonesia, baada ya nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia kusema kuwa haitampokea afisa huyo wa Washington. Baraza la Maulamaa la Indonesia jana Ijumaa lilitoa taarifa ya kupinga safari ya Jessica Stern, mjumbe maalumu wa Marekani katika masuala ya usenge, usagaji na…

Kombe la Dunia Qatar limeonyesha kufeli mpango wa kuanzisha uhusiano na Israel

Kombe la Dunia Qatar limeonyesha kufeli mpango wa kuanzisha uhusiano na Israel

Khatibu wa msikiti mtakatifu wa al-Aqswa huko Palestina amesema, wananchi wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu wanaoshuhudia mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Qatar wamethibitisha kugonga mwamba mpango mchafu wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel. Samahat Sheikh Ikrima Sabri sambamba na kuashiria msimamo sahihi unaoonyeshwa na Waislamu katika…

Jumuiya ya Walimu wa Qur’ani yaanzishwa nchini Mauritania

Jumuiya ya Walimu wa Qur’ani yaanzishwa nchini Mauritania

Jumuiya ya walimu na wataalamu wa Qur’ani Tukufu iliyoanzishwa nchini Mauritania ilianza shughuli zake katika sherehe iliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nouakchott. Inalenga kuandaa na kuratibu shughuli za walimu na wataalamu wa Qur’ani na kuboresha hali zao ili kuwahudumia vyema wanafunzi wa Qur’ani, msemaji wa shirika hilo alisema. Akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi,…