Vyombo vya Habari

Wapiganaji zaidi ya 40 wa Boko Haram waangamizwa Nigeria

Wapiganaji zaidi ya 40 wa Boko Haram waangamizwa Nigeria

Mkurugenzi wa Idara ya Habari ya Wizara ya Ulinzi ya Nigeria ametangaza mapema leo Jumamosi kwamba magaidi 44 wa kundi la Boko Haram wameuawa katika operesheni za anga na nchi kavu za jeshi kaskazini mwa nchi hiyo. Brig.-Gen Musa Danmadami ametangaza kuwa magaidi hao 44 wa Boko Haram waliuawa wiki iliyopita katika operesheni za jeshi la Nigeria…

Waingereza wafakamia chakula cha mifugo kutokana na kupanda gharama za maisha

Waingereza wafakamia chakula cha mifugo kutokana na kupanda gharama za maisha

Mgogoro wa gharama kubwa za maisha nchini Uingereza umekuwa sababu ya Waingereza katika baadhi ya miji kula chakula cha wanyama wa kufuga majumbani. Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kwamba wananchi “wanakula chakula cha wanyama” kwa sababu hawawezi kumudu chakula cha kawaida. Ripoti zinasema, baadhi ya maeneo ya Wales yamekumbwa na umaskini mkubwa kiasi kwamba watu…

Kizazi cha Waingereza weusi chapoteza imani kwa polisi wa nchi hiyo

Kizazi cha Waingereza weusi chapoteza imani kwa polisi wa nchi hiyo

Matokeo ya utafiti uliofanywa nchini Uingereza yanaonyesha kiwango kikubwa cha kutokuwa na imani kizazi cha vijana weusi wa nchi hiyo kwa polisi; Kwa kadiri kwamba hawataki hata kupiga simu polisi wakatii wa hatari. Kulingana na matokeo ya utafiti wa shirika la ushauri la Uingereza, Crest, asilimia 36 tu ya vijana weusi ndio waliosema kuwa wanawaamini polisi…

Kongamano la Kuala Lumpur kujadili Qur’ani Tukufu inavyoweza kutatua changamoto za kisasa

Kongamano la Kuala Lumpur kujadili Qur’ani Tukufu inavyoweza kutatua changamoto za kisasa

Kongamano limepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Malaysia Disemba 3 kujadili masuluhisho ya Qur’ani Tukufu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za siku hizi. Taasisi ya Warisan Ummah Ikhlas Foundation (WUIF) ndiyo inayoandaa hafla hiyo kwa kushirikisha wataalamu kutoka nchi kadhaa. Wazungumzaji watatoka Malaysia, Indonesia, Bangladesh, Misri, Marekani na Palestina. Ukumbi wa Perdana MTI huko…

Rais Samia: Wanawake milioni 44 wamepoteza ajira Afrika

Rais Samia: Wanawake milioni 44 wamepoteza ajira Afrika

Takwimu zinaonyesha wanawake milioni 44 wamepoteza ajira barani Afrika hadi kufikia mwaka 2021, huku idadi ya wanawake kwenye vyombo vya maamuzi Tanzania ikiongezeka kutoka asilimia 21.5 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 37 mwaka 2020. Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Desemba 3, 2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati akifungua kongamano…

Sheikh Ali Da’mush: Mshindi halisi wa Kombe la Dunia Qatar ni Palestina

Sheikh Ali Da’mush: Mshindi halisi wa Kombe la Dunia Qatar ni Palestina

Naibu wa Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mshindi halisi wa fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar ni taifa la Palestina kutokana na wimbi kubwa la wachezaji na mashabiki wa soka kuwaunga mkono wananchi wa Palestina. Sheikh Ali Da’mush amebainisha kuwa, matukio mbalimbali yanayoshuhudiwa hivi sasa katika mashindano…

Guterres: Dunia inaitegemea Afrika kutatua shida zake lakini haiisaidii Afrika kukabili changamoto zake

Guterres: Dunia inaitegemea Afrika kutatua shida zake lakini haiisaidii Afrika kukabili changamoto zake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema suala la kusikitisha ni kuwa, licha ya kwamba dunia inaitegemea Afrika kutatua shida zake, lakini bado bara la Afrika halijaweza kuweka tegemeo lake kwa dunia katika kukabili changamoto zinazolikabili. Guterres amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari, ambao umehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja…

Biashara baina ya Iran, Afrika yapindukia dola milioni 990 ndani ya miezi 7

Biashara baina ya Iran, Afrika yapindukia dola milioni 990 ndani ya miezi 7

Miamala ya kibiashara kati ya Jamhuri ya Kiislamu na nchi za Afrika imepindukia dola milioni 990 za Marekani katika kipindi cha miezi saba iliyopita. Hayo yameripotiwa na gazeti la Financial Tribune ambalo limeeleza kuwa, mabadilishano hayo ya biashara baina ya Iran na Afrika baina ya March 21 na Oktoba 22 ni tani milioni 1.89 zenye thamani ya dola 992.77….