Vyombo vya Habari

Askari 13,000 wa Ukraine wameuawa katika vita na Russia

Askari 13,000 wa Ukraine wameuawa katika vita na Russia

Mykhailo Podoliak, mshauri wa Rais wa Ukraine, amesema: vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo hadi sasa vimepoteza kati ya wanajeshi 10,000 hadi 13,000 katika vita dhidi ya Russia. Podoliak amesema katika mahojiano na Channel 24 TV ya Ukraine: “tuna takwimu rasmi kutoka kwa makao makuu ya ya Kamandi ya juu zinazoonyesha idadi hii ya wanajeshi…

Marekani yaiwekea vikwazo vipya Hizbullah ya Lebanon

Marekani yaiwekea vikwazo vipya Hizbullah ya Lebanon

Katika kuendeleza sera zake za mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon, serikali ya Marekani imewawekea vikwazo watu watatu na makampuni mawili ya Lebanon kwa kisingizio cha kutoa huduma za kifedha kwa harakati hiyo. Sambamba na hatua zake za kujaribu kupunguza mapenzi na umaarufu wa harakati ya Hizbullah nchini Lebanon, Washington imekuwa…

Bin Salman anaigeuza ardhi ya maeneo matakatifu ya Makka na Madina uwanja wa ufasiki wa kimaadili

Bin Salman anaigeuza ardhi ya maeneo matakatifu ya Makka na Madina uwanja wa ufasiki wa kimaadili

Mwandishi wa habari na mpinzani wa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia amekosoa kufanyika tamasha la muziki liitwalo MDLBEAST katika ardhi ya maeneo mawili matakatifu (Haramaini-Sharifaini) ya Makka na Madina na kueleza kwamba: Bin Salman anatoa huduma kubwa zaidi kwa maadui wa Uislamu kwa kuigeuza nchi hiyo kuwa uwanja wa kufanyia ufisadi wa kimaadili. Katika…

Sisitizo la Pakistan la kuendelea na misimamo yake dhidi ya Israel

Sisitizo la Pakistan la kuendelea na misimamo yake dhidi ya Israel

Waziri Mkuu wa Pakistan Muhammad Shahbaz Sharif ameitaja hali ya kutia wasiwasi inayoshuhudiwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kuwa ni changamo kubwa kwa amani na usalama duniani. Shahbaz Sharif pia amezitaja sera za kichokozi na kivamizi za utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi za Palestina na kutochukua hatua jamii ya kimataifa kuwa ndiyo…

Hamas: Wavamizi watateketea katika moto wa hujuma dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa

Hamas: Wavamizi watateketea katika moto wa hujuma dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imewatahadharisha Wazayuni kuhusu kuendelea kuuhujumu Msikiti wa al Aqsa na kuwatolea mwito Wapalestina kuhudhuria kwa nguvu zote na kwa mshikamano katika msikiti huo. Msikiti wa al Aqsa ambao ni nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na wa Palestina katika mji wa Baitul Muqaddas umekuwa ukilengwa na kukabiliwa…

Waziri: Ukimwi unaua Waganda 46 kila siku

Waziri: Ukimwi unaua Waganda 46 kila siku

Waziri katika Ofisi ya Rais nchini Uganda ameashiria ongezeko la maambukizi ya virusi vya HIV vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi miongoni mwa tabaka la vijana wanaobaleghe nchini humo na kusema kuwa, maradhi hayo yanaua Waganda 46 kwa siku. Milly Babalanda amesema hayo akinukuu takwimu za Wizara ya Afya ya Uganda zinazoonesha kuwa, asilimia 37 ya kesi…

Raisi: Iran daima inaunga mkono taifa lenye umoja na serikali yenye nguvu huko Iraq

Raisi: Iran daima inaunga mkono taifa lenye umoja na serikali yenye nguvu huko Iraq

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo kati yake na Waziri Mkuu wa Iraq hapa Tehran kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote inakaribisha na kuunga mkono taifa lenye mshikamano na serikali yenye nguvu huko Iraq. Mohammed Shia al Sudani Waziri Mkuu wa Iraq jana Jumanne aliwasili Tehran akiongoza ujumbe wa…

Malengo ya maadui ya kufuatilia kuligawa taifa la Iran

Malengo ya maadui ya kufuatilia kuligawa taifa la Iran

Baada ya hivi karibuni kuzuka vurugu na machafuko mapya nchini Iran maadui sugu wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu walichukua hatua ya kufuatilia senario ya kuligawa taifa hili katika kambi mbili. Katika senario hii, maadui wamejikita katika masuala mbalimbali. Senario hii kubwa inagawanywa pia katika nyuga nyingine ndogo zaidi mithili ya kikosi cha polisi, utawala,…