Baraza la Usalama labainisha wasiwasi wake juu ya kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema linatiwa wasiwasi na kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Tor Wennesland Mratibu Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani katika eneo la Asia Magharibi amebainisha wasiwasi wake kuhusu kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa…
Sensa Uingereza: Idadi ya Waislamu yaongezeka; Wakristo wazidi kupungua
Idadi ya Waislamu inazidi kuongezeka kwa kasi nchini Uingereza huku wafuasi wa dini ya Kikristo ikipungua katika taifa hilo la bara Ulaya. Takwimu za sensa ya makazi na watu zinaonyesha kuporomoka kwa idadi ya Wakristo nchini Uingereza na kwamba, chini ya nusu ya idadi ya watu England na Wales ni Wakristo. Kwa mujibu wa takwimu…
Juhudi za Mwanazuoni wa Kimisri za Kufafanua juu ya Hadhi ya Wanawake katika Qur’ani
Dkt. Fawzia al-Ashmawi alikuwa mwanazuoni ambaye alitumia maisha yake kueleza na kufafanua kuhusu hadhi ya wanawake katika Qur’ani Tukufu. Al-Ashmawi, ambaye alifariki mwezi uliopita, alikuwa msomi wa Misri, mwandishi, mfasiri na mtarjumi. Alifanya kazi kama Profesa wa fasihi ya Kiarabu na ustaarabu wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Geneva. Pia aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza…
Mchambuzi: Wafanyakazi wa Kiafrika wanakandamizwa sana Saudia
Haki za wafanyakazi wahamiaji wa Kiafrika zinapuuzwa kwa kiwango kikubwa Saudia Arabia na utawala huo wa kifalme wenye kiburi. Zaakir Ahmed Mayet alisema hayo katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Press TV siku ya Jumapili baada ya kanda za video kufichua mauaji ya wahajiri wa Kiafrika kutoka Ethiopia yanayofanywa na wanajeshi wa utawala wa…
Rais wa zamani wa Komoro Abdallah Sambi ahukumiwa kifungo cha maisha jela
Rais wa zamani wa visiwa vya Komoro Abdallah Sambi amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la uhaini mkubwa. Mahakama ya Usalama wa Taifa ya serikali ya Komoro ilitangaza jana wakati wa kusikilizwa kesi hiyo kwamba Ahmed Abdallah Sambi, rais wa zamani wa visiwa hivyo, ambaye alishtakiwa kwa uhaini, amehukumiwa kifungo cha maisha jela. Sambi alishtakiwa…
Kusambaratika siasa za vikwazo; Marekani yapigia magoti mafuta ya Venezuela
Baada ya kupita takriban miaka 10 ya vikwazo vikali vya Marekani dhidi ya Venezuela, hatimaye Washington imesalimu amri na imeamua kupigia magoti mafuta ya Venezuela. Marekani na waitifaki wake wakiwemo pia vibaraka wa ndani ya Venezuela, waliweka mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya serikali ya Caracas kwa shabaha ya kuipindua serikali hiyo na kupandikiza mfumo…
Kuna uhusiano upi baina ya dini uvumilivu au istiqama
Maisha ya watu yamejaa changamoto na magumu yasiyotarajiwa. Kila mtu, kwa kuzingatia hali na hadhi yake, hukabiliana na matatizo au masaibu mbalimbali ya kibinafsi, ya kifamilia na kijamii lakini si watu wote wanaoyavumilia na kuyastahimili vivyo hivyo. Hisia hasi, ambazo ni kati ya hisia kuu tunazokabiliana nazo maishani, huweka gharama kubwa kwa watu binafsi na…
Rais wa Algeria: Kuiunga mkono Palestina kusiishie kwenye utoaji taarifa tu
Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria amesisitiza haja ya kuchukuliwa hatua za kivitendo ili kurejesha haki za Wapalestina. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Tebboune, amezitaka nchi duniani kuchukua hatua za kivitendo za kuunga mkono haki za watu wa Palestina na akaeleza kwamba uungaji mkono huo haupasi kujifunga na utoaji msururu wa kauli na taarifa tu. Rais wa…