Vyombo vya Habari

Makamu wa Rais wa Malawi atiwa mbaroni kwa tuhuma za rushwa

Makamu wa Rais wa Malawi atiwa mbaroni kwa tuhuma za rushwa

Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima amejikutan matatani baada ya kutiwa mbaroni akikabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa. Taasisii ya kupambana na rushwa nchini Malawi imetangaza kuwa, kati ya Machi na Oktoba mwaka jana, makamu huyo wa Rais alipokea zaidi ya dola 280,000 na vitu vingine kama malipo baada ya kusaidia kampuni mbili kupewa…

Uungaji mkono wa Marekani kwa makundi yanayotaka kujitenga ya Iran

Uungaji mkono wa Marekani kwa makundi yanayotaka kujitenga ya Iran

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imelaani operesheni za kijeshi Iran dhidi ya makundi ya kigaidi ya Wakurdi wanaotaka kujitenga yaliyoko kaskazini mwa Iraq na imeitaka Tehran kusitisha mashambulizi hayo. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitoa taarifa hiyo baada ya Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) kutoa malalamiko yake kuhusiana na operesheni za kijeshi…

Wauguzi wa Uingereza kufanya mgomo mwezi ujao kudai malipo bora

Wauguzi wa Uingereza kufanya mgomo mwezi ujao kudai malipo bora

Wauguzi kote nchini Uingereza mwezi ujao watafanya mgomo ambao pamoja na mambo mengine unadai malipo bora. Mgomo huo ambao utakuwa wa kwanza katika historia ya miaka 106 ya chama chao cha wauguzi unatarajiwa kujumuisha wafanyakazi wengine wa Uingereza kuchukua hatua za kusimamisha kazi wakidai malipo bora. Wafanyakazi nchini Uingereza, Wales na Ireland ya Kaskazini  watafanya…

Umoja wa Mataifa: Video za kunyongwa wanajeshi wa Russia huko Ukraine ni za kweli

Umoja wa Mataifa: Video za kunyongwa wanajeshi wa Russia huko Ukraine ni za kweli

Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kwamba kuna uwezekani mkubwa kwamba video za kunyongwa wanajeshi wa Russia waliotekwa nyara huko Ukraine ni za kweli. Kulingana na shirika la habari la IRNA, Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, amesema katika taarifa yake kwamba matokeo ya…

Kombe la Dunia: Iran yaichapa Wales 2-0 na kuhuisha matumaini ya kusonga mbele

Kombe la Dunia: Iran yaichapa Wales 2-0 na kuhuisha matumaini ya kusonga mbele

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iimeichapa Wales mabao 2 kwa 0 katika fainali za mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Qatar. Vijana wa Kocha Mreno Carlos Queiroz leo waliingia uwanjani katika mechi ya kundi B wakiwa na jeraha kubwa la kutandikwa na Uingereza mabao 6 kwa…

Mgomo wa wahadhiri 70,000 katika vyuo 150 Uingereza kuathiri wanafunzi zaidi milioni 2.5

Mgomo wa wahadhiri 70,000 katika vyuo 150 Uingereza kuathiri wanafunzi zaidi milioni 2.5

Wahadhiri wa vyuo vikuu nchini Uingereza wameanzisha mgomo wa nchi nzima kulalamikia mishahara yao na mazingira ya kazi. Zaidi ya wahadhiri, watafiti na wakutubi elfu sabini wa vyuo vikuu 150 vya Uingereza wamefanya mgomo kwa siku tatu ulioanza jana Alhamisi na kuendelea leo Ijumaa kabla ya kurudiwa tena siku ya Jumatano ijayo, hatua ambayo itaathiri na kukwamisha masomo ya wanachuo…

Msahafu unaonasibishwa na Imam Ali waonyeshwa mjini Lahore

Msahafu unaonasibishwa na Imam Ali waonyeshwa mjini Lahore

Tamasha la Kimataifa la Sanaa ya Kiislamu, lililofanyika Lahore kwa kushirikisha nchi kadhaa za Kiislamu lilihitimishwa Jumapili. Iliangazia nyanja na nyanja tofauti za sanaa ya Kiislamu, pamoja na kaligrafia ya Kiislamu, Misahafu ya kale n.k. Moja ya sehemu kuu ilikuwa ni ile iliyoonyesha Misahafu adimu kurasa za maandishi ya Qur’ani yaliyoandikwa kwa mbinu ya mapambo…

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yaonuya kuhusiana na jinai za Israel dhidi ya Wapalestina

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yaonuya kuhusiana na jinai za Israel dhidi ya Wapalestina

Katibu Mkuuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ameonya kuhusiana na jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina na kueleza kwamba, zitakuwa na matokeo mabaya zaidi. Ahmad Abul-Gheit, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa, ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina uko…