Uingereza yakiri, silaha zinazopelekwa Ukraine kutwaliwa na magaidi
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kitaifa wa Jinai nchini Uingereza (NCA) amesema silaha zinazopelekwa Ukraine na nchi za Magharibi yumkini zikafanyiwa magendo na kuishia mikononi mwa magenge ya wahalifu na magaidi katika kona mbalimbali za dunia. Graeme Biggar amenukuliwa akisema hayo na gazeti la Sunday Times na kufafanua kuwa, “Katika mgogoro wowote ule, silaha zinapoingizwa…
Abdulsalam: Baadhi ya makundi ya Wayemen yanafaidika na kuendelea umwagaji damu
Mkuu wa ujumbe wa serikali ya uwokovu wa kitaifa ya Yemen katika mazungumzo ya amani ya nchi hiyo ameeleza kuwa, baadhi ya mirengo ya ndani huko Yemen yenye mfungamano na Riyadh yamegeuka na kuwa wafaidikaji katika vita huko Yemen. Saudi Arabia huku ikiungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi nyingine kadhaa mwezi Machi mwaka 2015…
Sisitizo la kuchunguzwa jinai za jeshi la Marekani nchini Afghanistan
Sambamba na kuanza uchunguzi kuhusiana na jinai za kivita nchini Afghanistan unaofanywa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetoa wito wa kuchunguzwa mashambulio ya mauaji ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan. Katika ripoti yake ya hivi karibuni, Human Rights Watch imetangaza kuwa, katika miaka…
Kombe la Dunia; Vijana wa Kiarabu wakataa kuzungumza na wanahabari wa Israel
Mashabiki wa soka wa nchi za Kiarabu wamekataa kuzungumza na waandishi wa habari wa masharika ya utawala haramu wa Israel nchini Qatar, kunakofanyika fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu 2022; kuonyesha upinzani wao wa kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala huo bandia unaokaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina. Vyombo vya habari vya Israel…
Rais wa Iran asema Marekani inashindwa kutokana na maendeleo ya Wairani lakini bado haijifunzi kutokana na hilo
Rais Ebrahim Raisi wa Iran amesema Marekani imeshindwa mbele ya maendeleo makubwa yaliyofanywa na taifa la Iran katika kipindi cha miongo minne iliyopita lakini bado haijajifunza kutokana na kushindwa kwake huko. “Ghadhabu na uadui wa Wamarekani kutokana na maendeleo ya taifa la Iran daima imeendelea bila natija katika miongo minne iliyopita, lakini Wamarekani bado hawajajifunza…
Vikwazo vilivyowekwa na al-Shabaab vyazidisha maafa ya kibinadamu nchini Somalia
Vikwazo vinavyoendelea kuwekwa na magaidi wa kundi la al-Shabaab katika baadhi ya maeneo ya Somalia vinazidisha hali mbaya ya kibinadamu katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. Bakool kusini magharibi mwa Somalia ni mojawapo ya mikoa iliyoathiriwa zaidi na ukame. Eneo hilo limekuwa chini ya vizuizi vya al-Shabaab kwa zaidi ya muongo mmoja, huku njia…
Waandamanaji wenye hasira wajaribu kuvamia ubalozi wa Ufaransa nchini Burkina Faso
Polisi nchini Burkina Faso walirusha mabomu ya kutoa machozi siku ya Ijumaa kuwatawanya waandamanaji waliokuwa na hasira waliojaribu kuvamia ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu Ouagadougou, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti. Waandamanaji hao waliokuwa wakitaka balozi wa Ufaransa nchini humo atimuliwe, walikusanyika katika uwanja wa manispaa asubuhi kabla ya kuelekea kwenye ubalozi wa Ufaransa,…
Waziri Mkuu wa Italia akosoa sera za ukoloni na unafiki wa Ufaransa kuhusu wahamiaji
Waziri Mkuu wa Italia ameikosoa hadharani Ufaransa kwa mtazamo wake wa kinafiki kuhusu suala la wahamiaji wanaotoka Afrika, ambalo limekuwa mzozo kati ya nchi hizo mbili katika wiki za karibuni huku akifichua sera ya ukoloni ya Paris huko Burkina Faso. Giorgia Meloni, ambaye alikuwa akizungumza katika mahojiano ya televisheni, ameyasema hayo huku akionyesha picha ya…