Kiongozi wa Korea Kaskazini: Tutatumia silaha za atomiki kujibu vitisho vya atomiki
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ameionya Marekani kuwa nchi yake itajibu vitisho vya atomiki kwa silaha za atomiki na makabiliano kwa makabiliano dhidi yake. Kim ametoa indhari hiyo wakati akisimamia jaribio la ufyatuaji wa kombora linalovuka bara moja kuelekea jengine aina ya Hwasong-17 na kusisitiza kuwa kitisho chochote cha kijeshi dhidi ya Pyongyang kitakabiliwa na…
Iraq yawatia nguvuni magaidi 15 wa Daesh
Vikosi vya usalama vya Iraq vimewatia mbaroni magaidi 15 wa kundi la Daesh katika mikoa sita ya nchi hiyo. Mamluki waliosalia wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wangali wanaendesha harakati zao katika mikoa ya Baghdad, Salahuddin, Diyala, Kirkuk, Nainawa na al Anbar huko Iraq. Idara ya Usalama wa Taifa ya Iraq jana Ijumaa…
Zaidi ya watoto wachanga 80 wanafariki kila siku mara baada ya kuzaliwa nchini Yemen
Afisa wa Wizara ya Afya ya Serikali ya Kitaifa ya Wokovu ya Yemen amesema zaidi ya watoto wachanga 80 hufa kila siku kutokana na ukosefu wa vifaa vya matibabu. Tangu kuanza kwa vita dhidi ya Yemen mwezi Machi 2015, muungano wa Saudia umeiwekea nchi hiyo mzingiro wa kila upande. Uhaba mkubwa wa fueli nchini Yemen…
Chanjo tatu za aina adimu ya Ebola ziko tayari huku Uganda ikipambana na mripuko wa ugonjwa huo
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO amesema kwamba, chanjo tatu za aina adimu ya ugonjwa wa Ebola inayoendelea kusambaa hivi sasa nchini Uganda zitapelekwa nchini humo kwa majaribio ya kizahanati. Dk. Matshidiso Moeti ameaambia waandishi wa habari kwamba chanjo hizo zitatumika katika mfumo unaojulikana kwa kimombo kama “ring vaccination trial”…
Mabadiliko ya hali ya hewa kusababisha mafuriko mabaya barani Afrika
Uchunguzi uliochapishwa na gazeti moja la Marekani umebaini kuwa kuna uwezekano wa kutokea mafuriko makubwa yatakayosababisha vifo vingi barani Afrika. Mtandao wa gazeti la Washington Post la Marekani umeripoti kuwa, watafiti wamefikia hitimisho kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na binadamu yameongeza uwezekano wa kunyesha mvua kubwa kupita kiasi itakayosababisha mafuriko mara 80 zaidi…
Abdollahian azihutubu Israel, Magharibi: Iran si Libya au Sudan
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema maadui wameelekeza mashambulizi yao dhidi ya ardhi na utambulisho wa Iran kwa kuunga mkono harakati za ugaidi ndani ya nchi; lakini njama hizo zimegonga mwamba kutokana na kusimama kidete Wairani. Hossein Amir-Abdollahian alisema hayo jana Alkhamisi katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa Twitter…
Mgogoro wa mafuta Ulaya, wananchi washambulia vituo vya mafuta Ufaransa
Madereva wa vyombo vya usafiri nchini Ufaransa wameshambulia vituo vya mafuta na kusababisha foleni kubwa baada ya bei ya bidhaa hiyo muhimu kupaa vibaya wakati huu wa mgogoro mkubwa wa nishati barani Ulaya. Televisheni ya Ruptly imeripoti habari hiyo leo na kuongeza kuwa, makumi ya madereva wa magari ya usafiri mjini Paris wamevamia vituo vya mafuta…
Kuongezeka mawazo ya kutaka kujiua miongoni mwa watoto na vijana wa Marekani
Matokeo ya utafiti uliofanya huko Marekani yanaonyesha kuwa mawazo na fikra za kutaka kujiua zimeongezeka sana kati ya watoto na vijana wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, matokeo ya utafiti huo yaliyochapishwa katika jarida la matibabu la Pediatrics yanaonyesha kuwa idadi ya watu wanaolazimika kufika katika…