Vyombo vya Habari

Indhari ya UNRWA kuhusu kuongezeka umaskini miongoni mwa wakimbizi wa Kipalestina

Indhari ya UNRWA kuhusu kuongezeka umaskini miongoni mwa wakimbizi wa Kipalestina

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) limetahadharisha kuhusu kuongezeka kwa kiasi kikubwa umaskini miongoni mwa wakimbizi wa Kipalestina huko Syria, Lebanon na Ukanda wa Ghaza. Wapalestina zaidi ya milioni 6 wanaishi kama wakimbizi katika nchi mbalimbali na hasa katika nchi zinazopakana na Palestina. Wakimbizi hao wa Kipalestina ambao kabla ya…

Timu ya kandanda ya Iran yawasili Qatar kushiriki Kombe la Dunia

Timu ya kandanda ya Iran yawasili Qatar kushiriki Kombe la Dunia

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewasili Doha, mji mkuu wa Qatar kwenda kuweka kambi ya kujianjdaa kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza kutifua mavumbi wiki ijayo. Wachezaji, wakufunzi na benchi la ufundi la timu hiyo imewasili Doha usiku wa kuamkia leo, tayari kwa mashindano hayo makubwa zaidi ya…

Vikwazo vipya vya Umoja wa Ulaya na Uingereza dhidi ya Iran; mkinzano wa vitendo na kaulimbiu

Vikwazo vipya vya Umoja wa Ulaya na Uingereza dhidi ya Iran; mkinzano wa vitendo na kaulimbiu

Jumatatu ya jana tarehe 14 Novemba, Umoja wa Ulaya na Uingereza zilitangaza kuiwekea vikwazo vipya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika hatua iliyopangwa na kuratibiwa baina ya pande mbili hizo. Uingereza imetangaza kuwaweka katika orodha yake ya vikwazo watu na taasisi 24 za Kiirani kwa kisingizio cha kile kilichoelezwa kuwa kukiuka haki za binadamu. Hatua…

Watu 24 wauawa katika mapigano ya kikabili Darfur Sudan

Watu 24 wauawa katika mapigano ya kikabili Darfur Sudan

Mapigano ya kikabila yaliyozuka katika eneo la Darfur huko Sudan yamesababisha vifo vya karibu watu 24 na kupelekea hali ya dharura kutangazwa eneo hilo. Kiongozi mmoja wa kikabila ameziambia duru za habari kwamba, nyumba zimeteketezwa na mali kuporwa na hali bado inasalia kuwa tete hata baada ya kuwasili kwa maafisa wa usalama wa serikali. Shirika…

Marekani yaongoza orodha ya nchi zinazofanya israfu ya chakula duniani

Marekani yaongoza orodha ya nchi zinazofanya israfu ya chakula duniani

Umoja wa Mataifa umesema jamii ya kimataifa haijachukua hatua za maana za kukomesha utupaji wa chakula majaani, huku Marekani, Australia na New Zealand zikiongoza orodha ya nchi zinazofanya israfu kubwa ya chakula duniani. Rosa Rolle, afisa mwandamizi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) amesema mataifa ya dunia yaliahidi mwaka 2015…

Uingereza yaazimia kuwaondoa askari wake nchini Mali

Uingereza yaazimia kuwaondoa askari wake nchini Mali

Uingereza imetangaza habari ya kutaka kuwaondoa mamia ya askari wa nchi hiyo walioko nchini Mali chini ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa MINUSMA. Waziri wa Vikosi vya Majeshi ya Uingereza, James Heappey ameliambia Bunge la nchi hiyo kuwa, serikali ya London haiwezi kuvumilia udhalilishaji wa nchi mwenyeji, ambayo eti haina azma ya kushirikiana…

UN: Idadi ya watu duniani yafika bilioni 8

UN: Idadi ya watu duniani yafika bilioni 8

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa jamii ya watu duniani leo Jumanne Novemba 15 imefikia watu bilioni 8. Kwa mujibu wa makadirio ya umoja huo, hii imetajwa kuwa hatua muhimu katika maendeleo ya mwanadamu kabla ya viwango vya kuzaana kuanza kupungua. Katika taarifa yake, Umoja wa Mataifa umesema kuwa, idadi hiyo inamaanisha watu bilioni 1 wameongezwa katika …

Vyama na makundi mbalimbali yatia saini hati maalumu ya kisiasa nchini Sudan

Vyama na makundi mbalimbali yatia saini hati maalumu ya kisiasa nchini Sudan

Vyama na makundi kadhaa ya kisiasa ambayo ni wanachama wa Muungano wa Uhuru na Mabadiliko wa Sudan yametia saini hati maalumu ya kisiasa inayokamilisha katiba mpya ya nchi hiyo Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Chama cha Ummah, Taasisi ya Ittihad, Baraza la Masuala ya Vyama vya Wafanyakazi Sudan, Muungano wa Kidemokrasia wa…