Vyombo vya Habari

Mkutano wa Rais wa Ufaransa na wanaoipinga Iran ni hatua ya kuchochea machafuko

Mkutano wa Rais wa Ufaransa na wanaoipinga Iran ni hatua ya kuchochea machafuko

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani kikao cha Rais wa Ufaransa na wapinzani wa Iran na kukitaja kitendo hicho kuwa ni ukiukaji mkubwa wa majukumu ya kimataifa ya Ufaransa katika kupambana na ugaidi na ukatili. Katika wiki za hivi karibuni, maafisa wa utawala wa Ufaransa wameingilia wazi wazi masuala ya ndani ya…

Marekani yaitaka Ukraine ifanye mazungumzo ya amani na Russia

Marekani yaitaka Ukraine ifanye mazungumzo ya amani na Russia

Maafisa wa ngazi za juu wa Marekani wameanzisha kampeni ya kuishawishi Ukraine itafakari juu ya suala la kufanya mazungumzo ya amani na Russia, wakihofia kuwa msimu wa baridi kali yumkini ukaikwamisha serikali ya Kiev baada ya eti kupata ushindi wa kulidhibiti tena eneo la Kherson. Gazeti la The Wall Street Journal la Marekani limeripoti kuwa,…

Hizbullah: Marekani imekusudia kuingamiza kabisa Lebanon

Hizbullah: Marekani imekusudia kuingamiza kabisa Lebanon

Naibu wa Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani inapanga njama za kuiangamiza kabisa kabisa Lebanon. Tovuti ya al Nashra imeripoti habari hiyo na kumnukuu Sheikh Ali Da’mush akisema hayo jana Jumapili na kusisitiza kuwa, muqawama hivi sasa ni imara na una nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wowote na kwa…

Bidhaa za Iran zinazidi kupata umaarufu barani Afrika

Bidhaa za Iran zinazidi kupata umaarufu barani Afrika

Kaimu Mkuu wa Kituo cha Biashara ya Iran na Afrika amesema: “Inatabiriwa kuwa kwa kasi ya sasa ya ustawi wa biashara ya Iran na Afrika katika mwaka huu (1401 Hijria Shamsia) kiwango cha mauzo ya bidhaa za Iran barani Afrika kitafika dola bilioni 1.8. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA, Sayyid Ruhullah Latifi,…

Mabaharia 16 Wairani waachiliwa huru Tanzania

Mabaharia 16 Wairani waachiliwa huru Tanzania

Mabaharia 16 Wairani waliokuwa wanashikiliwa nchini Tanzania wameachiliwa huru hivi karibuni. Hayo yamedokezwa na Mkuu wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran katika Eneo la Biashara Huria la Chabahar katika mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini-mashariki mwa Iran ambaye amesema mabaharia hao walioachiliwa huru ni wenyeji wa mkoa wa Sistan na Baluchestan….

Waasi wa Tigray kuweka silaha chini iwapo askari wa Eritrea wataondoka Ethiopia

Waasi wa Tigray kuweka silaha chini iwapo askari wa Eritrea wataondoka Ethiopia

Serikali ya Ethiopia na makamanda wa Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray (TPLF) wameafikiana kuweka silaha chini, mara tu wanajeshi wa nchi jirani ya Eritrea watakapoondoka nchini humo. Makubaliano hayo ya kuweka silaha chini na kuanisha njia za utekelezaji wa mapatano ya kudumu yaliyofikiwa Afrika Kusini hivi karibuni, yametiwa saini huko Nairobi, mji mkuu wa…

Kundi la kwanza la wanajeshi wa Kenya latua mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Kundi la kwanza la wanajeshi wa Kenya latua mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Wanajeshi wa Kenya jana Jumamosi walitua katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo’ ambapo walilakiwa na maafisa husika na wanajeshi wa Kongo katika eneo. Wanajeshi wa Kenya wamewasili katika mji wa Goma wakati kundi la waasi la M23 likiwa limeingia katika jimbo la Kivu Kaskazini la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na…

Trump: Wademokrat wameshinda Seneti kwa kuchakachua

Trump: Wademokrat wameshinda Seneti kwa kuchakachua

Rais wa zamani wa Marekani ametangaza kuwa chama cha Democratic kimeshinda uchaguzi wa Baraza la Seneti kwa udanganyifu katika uchaguzi wa katikati ya muhula uliofanyika hivi majuzi nchini humo. Baada ya Wademokrat kupata ushindi katika uchaguzi wa Seneti na kupata wingi wa kura katika chombo hicho cha kutunga sheria nchini Marekani, Donald Trump, rais wa zamani…