Afisa wa jeshi la Marekani: Karibuni hivi tutaingia kwenye mapigano ya muda mrefu na China
Afisa mwandamizi wa jeshi la Marekani amesema karibuni hivi nchi hiyo itaingia kwenye mzozo na makabiliano ya muda mrefu na China na akatahadharisha juu ya kile alichoeleza kuwa ni kubaki nyuma Washington katika uwezo wa kijeshi mkabala na Beijing. Adimeri Charles Richard, mkuu wa Kamandi ya Kimkakati ya Jeshi la Wanamaji la Marekani, ametahadharisha kuwa,…
Mzayuni aangamizwa katika operesheni ya wanamapambano wa Palestina
Kanali ya televisheni ya KAN ya utawala wa Kizayuni, mapema leo Jumanne imetangaza habari ya kuangamizwa mlowezi mmoja Mzayuni anayejulikana kwa jina la Shalom Sofer ambaye alijeruhiwa katika operesheni moja ya mwanamapambano wa Palestina. Televisheni hiyo imetangaza kuwa, Shalom Sofer alikuwa mlowezi wa Kizayuni anayeishi katika kitongoji cha Kedumim cha walowezi wa Kizayuni kilichojengwa kwenye ardhi…
Mtoto wa Rais Museveni atangaza kuliunga mkono kundi la waasi wa M23
Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema kwamba kundi la waasi la M23, linalopigana vita na jeshi la serikali ya Kinshasa, lina haki ya kufanya hivyo. Muhoozi ameandika katika ujumbe wa twitter akisema kwamba “ni hatari sana kwa mtu yeyote kupiga vita ndugu zetu. Sio magaidi, bali wanapigania haki za…
Faili la sauti lililovuja la mwandishi wa BBC: Lengo la machafuko ni kuigawa Iran
Faili la sauti lililovuja la mwandishi wa shirika la utangazaji la Uingereza BBC limefichua wazi jinsi Magharibi na vyombo vyao vya habari zinavyotekeleza njama ya kuigawa Iran. Maandamano yaliyoibuka hivi karibuni nchini Iran kwa kisingizio cha kifo cha “Mahsa Amini” kwa mara nyingine tena yamewafanya maadui wa kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutumia…
Biden apatwa na wahka: Nitauzuliwa iwapo Warepublican watashinda uchaguzi
Rais wa Marekani amekiri kwamba atakabiliwa na hatari ya kuitwa bungeni kwa ajili ya kusailiwa na kutimuliwa iwapo Warepublican watachukua udhibiti wa Bunge la Congress katika uchaguzi wa katikati ya muhula. Rais wa Marekani, Joe Biden, amekiri kwamba iwapo Warepublican watashinda uchaguzi huo na kulidhibiti Bunge la Congress Jumanne ya kesho, yumkini akasailiwa na kutimuliwa. Biden ametoa…
Msururu wa hukumu za vifo na kunyonga watu kwa halaiki; rekodi ya jinai aliyojiwekea Bin Salman
Shirika la Haki za Kibinadamu la Saudi Arabia lenye makao yake Ulaya limefichua kuwa viongozi wa utawala wa Riyadh wametoa hukumu ya kifo kwa wafungwa 15 walioshtakiwa kwa masuala ya kiitikadi, na kwamba kwa kutolewa hukumu hizo, idadi ya watu walio hatarini kunyongwa nchini humo imefika 53, wanane miongoni mwao wakiwa ni vijana chipukizi na…
Iran yazindua makombora mapya ya Bavar 373 na Sayyad B4
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua mfumo mpya wa makombora ya kujihami ya masafa marefu ya Bavar (Kujiamini) 373 na pia imefanyia majaribio kombora jipya la Sayyyad B4 leo Jumapili. Mfumo wa Bavar-373 wa makombora ya kijihami yenye uwezo wa kuruka umbali wa kilomita 300 umezinduliwa sambamba na kuanza uundwaji kwa wingi makombora ya Sayyad…
Shirika la Ndege la Kenya kuwapiga kalamu marubani waliogoma
Makumi ya maelfu ya wasafiri wa ndani na nje ya nchi wameachwa katika njiapanda katika viwanja vya ndege vya Kenya, baada ya safari zao kukatizwa kutokana na mgomo wa marubani wa Shirika la Ndege la Kenya Airways (KQ). Zaidi ya wasafiri 15,000 wameathiriwa na mgomo huo uliosimamisha safari zaidi ya 53 za ndani na nje ya…