Wauguzi wa Uingereza Uwapiga kura kugoma kutokana na ugumu wa maisha
Wauguzi wa Uingereza wamepiga kura kwa mara ya kwanza kugoma kitaifa kiviwanda kabla ya Krismasi, kwani kuongezeka kwa kiwango cha mfumuko wa bei kumewaingiza Waingereza wengi katika hali mbaya ya kiuchumi. Maafisa wa vyama vya wafanyakazi wanasema wauguzi katika “maeneo mengi ya ya nchi” wanaofanya kazi katika majimbo ya England, Scotland, Wales na Ireland Kaskazini…
Ndege ya abiria yaanguka Tanzania; watu 19 wathibitishwa kuaga dunia
Kwa akali watu 19 wameaga dunia nchini Tanzania, baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Precision Air kuanguka katika Ziwa Victoria jiirani kabisa na uwanja wa ndege wa Bukoba. Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila idadi ya waliofariki imefikia 19, majeruhi 26. Ndege ya Shirika la Ndege ya Precision Air…
Wakongo wafanya mandamano makubwa dhidi ya waasi wa M23 mjini Bukavu
Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wenye hasira wamechoma moto bendera ya Umoja wa Ulaya katika mji wa Bukavu mashariki mwa nchi hiyo, huku mamia ya wakiandamana dhidi ya waasi wa M23. Wananchi hao wameeleza kutoridhishwa kwao na uingiliaji wa mataifa makubwa kama vile Marekani, Uingereza na Ufaransa katika masuala ya ndani ya nchi…
Onyo la Russia kuhusu Wamagharibi kutuma magaidi nchini Ukraine
Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia, Nikolay Patrushev, ametangaza kuwa Marekani na Uingereza zinasajili na kuajiri magaidi wa kimataifa kwa ajili ya kushirikiana na jeshi la Ukraine katika vita dhidi ya Russia. Patrushev, ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa makatibu wa Baraza la Usalama la Jumuiya ya Madola Huru (CIS) siku ya…
Uingereza yalegeza kamba, yaghairi kuuhamishia ubalozi wake Baitul Muqaddas
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa serikali mpya ya Uingereza imelegeza kamba kuhusiana na mpango wa serikali ya waziri mkuu wa zamani Liz Truss wa kuhamishia ubalozi wa nchi hiyo katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu. Tarehe 22 Septemba, wakati Liz Truss alipokutana na waziri mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel…
Raisi: Hakuna jambo linaloweza kifanyika Asia Magharibi bila ya mwafaka wa Iran
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini taifa kubwa la Iran liliweka mapambano dhidi ya dhulma na ukoloni katika ajenda yake na kuongeza kuwa: “Hakuna mlingano unaoweza kufikiwa katika kanda ya Magharibi mwa Asia bila ya kupasishwa na Iran.” Rais Ebrahim Raisi ameyasema hayo leo katika…
Azimio la mwisho la maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana Ubeberu
Washiriki katika maandamano ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu inayosadifiana na leo 4 Novemba, wamesisitiza udharura kuwepo mapambano endelevu dhidi ya njama za kuzusha fitna, ghasia na fujo. Washiriki katika maandamano ya leo ya kupinga ubeberu wa kimataifa ambao walikuwa wakipiga nara za “Mauti kwa Marekani” kuonyesha kuchukizwa kwao na siasa za kiuadui…
Sheikh Isa Qassim: Uchaguzi ujao unalenga kuimarisha udikteta Bahrain
Kiongozi mashuhuri wa kidini nchini Bahrain amesema uchaguzi ujao wa Bunge nchini humo hauna lengo jingine isipokuwa kuimarisha mienendo ya kiimla na kidikteta ya watawala wa Aal-Khalifa. Sheikh Isa Qassim, kiongozi wa kidini wa mapinduzi ya Bahrain amesema hayo katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter hapo jana na kuongeza kuwa: Chaguzi nchini…