Maandamano Uingereza kulaani polisi wanaowaua watu wenye asili ya Afrika
Maandamano makubwa yamefanyika katika mji mkuu wa Uingereza, London, kupinga ubaguzi wa rangi ulivyokita mizizi katika jeshi la polisi nchini humo. Waandamanaji waliokuwa na hasira walifika katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza ili kuufahamisha umma kuhusu visa vya kutisha vya namna ambavyo, vijana ambao aghalabu wana asili ya Afrika wanavyopoteza maisha katika mazingira ya…
Mageuzi ya Bin Salman huko Saudi Arabia ni ya uongo na bandia
“Rima bint Bandar Al Saud”, balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani, alitangaza karibuni katika mahojiano na CNN, kwamba mageuzi ya Saudi Arabia ni ya kweli na kwamba ufalme huo umechukua hatua katika miaka mitano iliyopita ambayo ilikuwa haijafanyika katika miaka 80 iliyopita Katika kujibu matamshi hayo, Shirika la Haki za Kibinadamu la Ulaya-Saudia limetaja mageuzi…
Marekani na mchezo wa “chaguo la mwisho” nchini Iran Uwekezaji wa Washington katika ugaidi ni anguko la bure
Katika uchambuzi, gazeti la “Rai El Youm” sambamba na kuashiria nafasi ya Marekani katika shambulio la kigaidi mjini Shiraz, limeutaja ugaidi wa Washington kuwa ni chaguo la mwisho dhidi ya Iran na kubainisha kuwa, uwekezaji wa Ikulu ya Marekani kwa magaidi ni anguko la bure. Katika barua iliyoandikwa na Hasna Nasr al-Hussein, mchambuzi mwandamizi wa…
DNA yamuokoa Mmarekani mweusi aliyefungwa ‘kimakosa’ miaka 38
Raia mmoja wa Marekani mwenye asili ya Afrika ameachiwa huru baada ya kufungwa jela kwa karibu miongo minne kwa kosa ambalo hakulifanya. Maurice Hastings, 69, aliachiwa huru jana Ijumaa katika jimbo la California , baada ya vipimo vya msimbojeni (DNA) kuonesha kuwa hakuhusika na kosa la mauaji aliyodaiwa kufanya. Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ya Kaunti ya Los…
Kampuni ya Uingereza yagundulika kuhusika na kashfa ya kueneza saratani Iraq
Tovuti moja ya habari mefichua kuwa kampuni ya Uingereza inayofanya kazi katika maeneo ya mafuta ya Iraq ni moja ya sababu kuu za kuenea kwa saratani nchini humo. Tovuti moja ya habari imefichua kwamba Kampuni ya Petroli ya Uingereza ilisababisha kuenea kwa uugonjwa wa saratani nchini Iraq, lakini vyombo vya habari vya Magharibi na hasa vya…
Hifadhi ya gesi ya Uingereza zimebaki siku 9 pekee/London inataka kusimamisha msaada kutoka nje
Ripoti za vyombo vya habari vya Uingereza zinaonyesha kuwa hifadhi ya gesi ya Uingereza itadumu kwa siku tisa pekee, na kwamba waziri mkuu mpya wa nchi hiyo anafikiria kusimamisha ufadhili wa misaada ya kigeni ikiwa ni miongoni mwa juhudi za kupunguza gharama. Vyombo vya habari vya Uingereza vinaripoti kwamba akiba ya gesi ya Uingereza inatosha…
Afrika Kusini yaishambulia US kwa kutoa ‘tahadhari ya shambulio la kigaidi’
Viongozi wa Afrika Kusini wameikosoa serikali ya Marekani kwa kutoa tahadhari ya uwezekano wa kutokea shambulizi la kigaidi katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika. Jana Ijumaa, Idara ya Taifa ya Operesheni za Pamoja na Intelijensia ya Afrika Kusini (Natjoints) iliwaonya wananchi wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika dhidi ya kusambaza taarifa za uwongo…
Mashtaka rasmi ya Russia kwa Umoja wa Mataifa kuhusu maabara za silaha za kibiolojia za Marekani nchini Ukraine
Russia imepeleka malalamiko yake rasmi kwa Umoja wa Mataifa kuhusu kuwepo kwa maabara za silaha za kibiolojia za Marekani nchini Ukraine. Vasily Nebenzia, mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa, amethibitisha kwamba nchi yake imekusanya ushahidi wa kutosha kuhusu uwepo wa maabara ya silaha hizo za kibiolojia za Marekani huko Ukraine. Kwa kutuma…