Vyombo vya Habari

Ukosoaji mkali wa Putin kwa mauaji ya kigaidi ya shahidi Luteni Jenerali Soleimani

Ukosoaji mkali wa Putin kwa mauaji ya kigaidi ya shahidi Luteni Jenerali Soleimani

Akizungumza juzi Alhamisi katika Kongamano la Valdai, Rais Vladmir Putin wa Russia amekosoa mfumo na siasa za Magharibi na kueleza kuwa nchi za Magharibi zilimuua Luteni Jenerali Soleimani; katika hali ambayo shakhsia huyo alikuwa kiongozi rasmi nchini mwake na kuongeza kwamba Wamagharibi si tu hawajakana jambo hilo bali wanajifakharisha nalo. Putin amesema: “Wao ndio walimuua…

Russia: Marekani na Ulaya zinataka kuwafanya walimwengu waghafilike na kadhia ya Palestina

Russia: Marekani na Ulaya zinataka kuwafanya walimwengu waghafilike na kadhia ya Palestina

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Marekani na Ulaya ndio wahusika wakuu wa kushadidi mgogoro wa Palestina. Vasily Nebenzya, Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, umewadia wakati sasa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchuukua hatua za kurekebisha hali…

Mashirika ya kijasusi ya kigeni yakiongozwa na CIA yamehusika na ghasia Iran

Mashirika ya kijasusi ya kigeni yakiongozwa na CIA yamehusika na ghasia Iran

Taarifa ya pamoja ya Wizara ya Intelijensia ya Iran na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imesema mashirika ajinabi ya kijasusi yakiongozwa na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) yamekuwa na mchango mkubwa katika kupanga na kuratibu ghasia na fujo zilizoshuhudiwa hapa nchini kwa wiki kadhaa. Taarifa hiyo imesema CIA ya Marekani ilikuwa…

Zelensky alithamini ushirikiano wa kijasusi wa Tel Aviv

Zelensky alithamini ushirikiano wa kijasusi wa Tel Aviv

Rais wa Ukraine alidai ushirikiano wa kiintelijensia na utawala wa Kizayuni kuhusiana na ndege zisizo na rubani za Urusi na kuthamini msaada wa Tel Aviv. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alielezea hali ya uhusiano kati ya Kyiv na utawala wa Kizayuni kuwa “mwelekeo mzuri” na kushukuru ushirikiano wa kijasusi kati ya pande hizo mbili. Kulingana…

Somalia yataka isaidiwe na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuimarisha mifumo yake ya mahakama

Somalia yataka isaidiwe na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuimarisha mifumo yake ya mahakama

Jaji Mkuu wa Somalia amewasilisha ombi maalumu Kwa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuisaidia Somalia kuimarisha mifumo ya kimahakama ambayo imeathiriwa vibaya na vita hatua itakayoharakisha mchakato unaoendelea wa nchi hiyo wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Yusuph Bashe Mohamed Jaji Mkuu wa Somalia amewasilisha ombi hilo katika Mkutano wa pili wa Majaji…

Shambulio la kigaidi katika Haram ya Shah Cheragh; mfano mwingine wa mradi wa kuvuruga usalama wa Iran

Shambulio la kigaidi katika Haram ya Shah Cheragh; mfano mwingine wa mradi wa kuvuruga usalama wa Iran

Ikiwa ni katika kuendeleza mradi wa maadui wa kuvuruga usalama na kuibua machafuko nchini Iran, siku ya Jumatano idadi kubwa ya wafanyaziara katika Haram takatifu ya Ahmad bin Musa (as) huko katika mji wa Shiraz waliuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia shambulio la kigaidi lililotekelezwa katika haram hiyo. Jumatano alasiri gaidi mmoja wa kundi…

Mawaziri wa Uganda waanza kujifunza Kiswahili

Mawaziri wa Uganda waanza kujifunza Kiswahili

Mawaziri wa Uganda wameazimia kuanza kujifundisha lugha ya Kiswahili, ambayo mbali na kuwa lugha ya kitaifa, lakini pia ni lugha rasmi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Uganda hivi karibuni iliidhinisha Kiswahili kuwa lugha rasmi ya pili nchini humo baada ya Kiingereza, na kuifanya lugha hiyo kuwa ya lazima kufundishwa mashuleni. Makamu wa Kwanza wa…

Sisitizo la Iran la kutotumiwa droni zake katika vita vya Ukraine na kuwa tayari kuchunguza madai ya nchi hiyo

Sisitizo la Iran la kutotumiwa droni zake katika vita vya Ukraine na kuwa tayari kuchunguza madai ya nchi hiyo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema, Tehran iko tayari kuchunguza madai ya serikali ya Ukraine kuhusu kutumiwa na Russia ndege zisizo na rubani za Iran katika vita vya Ukraine. Amir-Abdollahian aliyasema hayo jana Jumatano baada ya mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus Vladimir…