Vyombo vya Habari

Takwa la Umoja wa Afrika kwa Wamagharibi la kuamiliana kwa heshima na mataifa masikini

Takwa la Umoja wa Afrika kwa Wamagharibi la kuamiliana kwa heshima na mataifa masikini

Kupamba moto vita vya Russia na Ukraine na kusambaa mgogoro wa kiuchumi katika akthari ya mataifa ya dunia, kumezifanya nchi za Kiafrika zitengwe na kutupwa mkono zaidi. Hali hii imezifanya nchi nyingi za bara hilo zikabiliwe na tatizo la kushindwa kujidhaminia mahitaji muhimu kama chakula na dawa. Kuhusiana na hilo, Rais wa Senegal, ambaye ndiye…

Syria: Tunataka uanzishwe mfumo mpya wa kimataifa, jinai za Israel zidhibitiwe

Syria: Tunataka uanzishwe mfumo mpya wa kimataifa, jinai za Israel zidhibitiwe

Kwa mnasaba wa Siku ya Umoja wa Mataifa, Serikali ya Syria imetoa wito na kusisitiza ulazima wa kuundwa mfumo mpya wa kimataifa na kuzuiwa uchokozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na jinai zinazofanywa na utawala huo haramu. Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Al-Akhbariya; Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetoa taarifa…

IOM: Idadi ya vifo vya wahajiri kuelekea Ulaya imeongezeka zaidi mwaka huu

IOM: Idadi ya vifo vya wahajiri kuelekea Ulaya imeongezeka zaidi mwaka huu

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kwamba idadi ya vifo vya watu wanaotafuta hifadhi imeongezeka kwa kiasi kikubwa kwenye njia za nchi kavu na baharini kuelekea Ulaya ikilinganishwa na mwaka jana. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza mjini Berlin kuwa watu wasiopungua 5,684 wamefariki dunia wakijaribu kukimbilia Ulaya kati ya Agosti 2021 na Septemba…

Wachambuzi wa mambo Tanzania wapokea kwa hisia mseto makabidhiano ya ripoti ya kikosi kazi

Wachambuzi wa mambo Tanzania wapokea kwa hisia mseto makabidhiano ya ripoti ya kikosi kazi

Wachambuzi wa mambo nchini Tanzania wamepokea kwa hisia mseto mapendekezo ya ripoti ya kikosi kazi kuhusiana na suala zima la demokrasia katika nchi hiyo. Maoni hayo yametolea baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupokea majuzi ripoti ya mapendekezo ya kikosi kazi kuhusu uratibu wa maoni ya wadau wa Demokrasia…

Maandamano ya Ulaya dhidi ya kuzorota hali ya kiuchumi

Maandamano ya Ulaya dhidi ya kuzorota hali ya kiuchumi

Kufuatia kuenea mgogoro wa kiuchumi katika nchi mbalimbali za Ulaya, wananchi wengi wameandamana katika nchi kama vile Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Romania kulalamikia hali mbaya ya maisha. Kuongezeka kwa gharama ya maisha, matatizo ya nishati na wasiwasi unaosababishwa na msimu ujao wa baridi kali pamoja na ongezeko la ushuru na ukosefu wa huduma ni kati…

Mashariki mwa Ulaya inakabiliwa na janga la ufukara wa nishati na hewa chafu

Mashariki mwa Ulaya inakabiliwa na janga la ufukara wa nishati na hewa chafu

Gazeti moja la Uingereza limeandika kuwa, wananchi wa maeneo ya mashariki mwa Ulaya wana utajiri mkubwa wa nishati ya bei nafuu lakini unasababisha uchafuzi mkubwa wa hali ya hewa. Utajiri huo ni kama ule wa makaa ya mawe ya rangi ya kahawia. Gazeti la Financial Times la Uingereza limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wananchi kama…

HAMAS: Utawala wa Kizayuni umeshindwa kukabiliana na muqawama Ukingo wa Magharibi

HAMAS: Utawala wa Kizayuni umeshindwa kukabiliana na muqawama Ukingo wa Magharibi

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, jinai za utawala wa Kizayuni za kuwaua kigaidi wanamapambano wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan hazitapunguza kasi ya kuimarika muqawama wa wananchi wa Palestina. Jana Jumapili, utawala wa Kizayuni ulimuua kigaidi Tamer al-Kilani, mmoja wa makamanda wa muqawama wanaojulikana kwa jina…

Murtadi Salman Rushdie apoteza jicho, apooza mkono baada ya kushambuliwa

Murtadi Salman Rushdie apoteza jicho, apooza mkono baada ya kushambuliwa

Duru moja ya kuaminika imesema kuwa, Salman Rushdie alipata majeraha makubwa katika shambulio la mwezi Agosti na amepoteza uwezo wa kuona jicho lake moja huku mkono wake mmoja nao ukiwa umepooza. Andrew Wylie ameliambia gazeti la lugha ya Kihispania la “El Pais” kwamba Rushdie, ambaye ana umri wa miaka 75, amepata madhara makubwa katika shambuliio…