Vyombo vya Habari

Erdogan: Kampuni ya Ufaransa ya Lafarge inaunga mkono ugaidi

Erdogan: Kampuni ya Ufaransa ya Lafarge inaunga mkono ugaidi

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kampuni kubwa ya saruji ya Ufaransa ya Lafarge sasa imefichuliwa kuwa moja ya taasisi muhimu zinazounga mkono ugaidi. Akizungumza katika  Mkutano wa 12 wa Mawaziri wa Habari wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ulioanza Ijumaa na kumalizika jana mjini Istanbul, Erdogan ameongeza kuwa, “Niliposema jinsi kampuni kubwa ya…

Xi Jinping achaguliwa kuendelea kuiongoza China

Xi Jinping achaguliwa kuendelea kuiongoza China

Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimemchagua Xi Jinping kuendelea kuwa katibu wake mkuu kwa muhula wa tatu katika kikao kilichomalizika jana na hivyo kumuidhinisha kuendelea kuwa rais wa China. Kikao cha 20 cha Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kimefanyika mapema leo chini ya uwenyekiti wa Xi. Wanachama pia walimchakuwa Xi kuwa…

Wanajeshi 176 wa Marekani walijiua mwaka 2021

Wanajeshi 176 wa Marekani walijiua mwaka 2021

Idadi ya askari wanaojiua katika Jeshi la Marekani imezidi kuongezeka mwaka uliopita wa 2021 ambapo takwimu zinaonyesha kuwa askari 176 walijiua. Takwimu hizo za Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, zinaonyesha kuwa, jeshi hilo limekuwa likijaribu kutafuta njia za kuimarisha kiwango cha maisha ya askari ili kuboresha afya yao ya kiakili. Tovuti ya military.com pia…

Maelfu waandamana nchini Ethiopia kupinga uingiliaji wa Marekani nchini humo

Maelfu waandamana nchini Ethiopia kupinga uingiliaji wa Marekani nchini humo

Maelfu ya Waethiopia walifanya maandamano ya nchi nzima siku ya Jumamosi kulaani kile walichokitaja kama uingiliaji wa madola ya kigeni, hasa Marekani, katika masuala ya ndani ya nchi yao. Katika mji mkuu Addis Ababa, waandamanaji walibeba mabango yaliyosomeka “Tishio kwa Ethiopia ni tishio kwa ulimwengu” na “heshimu uhuru wa kujitawala Ethiopia.” Mabango mengine yalikuwa na…

Kushambuliwa bandari ya al Dabah, onyo la Wayemen kwa wezi na waporaji wa mafuta

Kushambuliwa bandari ya al Dabah, onyo la Wayemen kwa wezi na waporaji wa mafuta

Ijumaa ya tarehe 21 Oktoba 2022, jeshi la Yemen lilitumia droni zake kushambulia bandari ya al Dabah huko Hadhramaut likiwa ni pigo jipya kwa wavamizi na onyo kwa madola vamizi yanayoongozwa na Saudi Arabia ambayo yanaendelea kupora utajiri wa nchi hiyo maskini zaidi ya Kiarabu. Al Dabah ni bandari muhimu katika mkoa wa Hadhramaut wa…

Uturuki yataka vikwazo dhidi ya Iran na Venezuela viondolewe ili kupunguza bei ya mafuta duniani

Uturuki yataka vikwazo dhidi ya Iran na Venezuela viondolewe ili kupunguza bei ya mafuta duniani

Uturuki imetoa wito wa kuondolewa vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Iran na Venezuela huku kukiwa na mzozo wa nishati duniani uliochochewa na oparesheni ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine. Ongezeko la bei ya nishati hasa petrol na gesi duniani ni chanzo cha kupanda gharama ya maisha kwa mamia ya mamilioni ya watu duniani…

Nyaraka nyeti zinazohusiana na Iran zimekutwa kwenye makazi ya Trump Florida

Nyaraka nyeti zinazohusiana na Iran zimekutwa kwenye makazi ya Trump Florida

Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa nyaraka nyeti zinazohusiana na Iran zimekutwa nyumbani kwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump. Tarehe 8 Agosti, maafisa ya Polisi ya Upelelezi ya Marekani FBI walivamia makazi ya Trump ya Mar- a-lago mjini Florida na kunasa maboksi 33 ya nyaraka, yakiwemo 11 yenye nyaraka nyeti za siri. Imeelezwa kuwa…

Saudia yamfunga jela daktari Mtunisia kwa kuweka video tu ya Watunisia kuhusu Hizbullah

Saudia yamfunga jela daktari Mtunisia kwa kuweka video tu ya Watunisia kuhusu Hizbullah

Saudi Arabia imemfunga jela miaka 15 daktari mmoja wa kike raia wa Tunisia kwa kuweka video ya maandamano ya kuiunga mkono Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon huko Tunisia. Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, mahakama moja nchini Saudia imemuhukumu kifungo cha miaka 15 jela Bi Mahdiyah al Barzouqi kwa madai ya…