OIC yatahadharisha kuhusu ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Hissein Brahim Taha ameelezea wasiwasi wa jumuiya hiyo kuhusiana na kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu katika baadhi ya nchi za Ulaya. Kikundi cha Mawasiliano kuhusu Waislamu barani Ulaya cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kimefanya mkutano wa wazi mjini New York, kando ya Kikao…
Vikwazo, ugaidi, vita na umwagaji damu; matokeo ya uchukuaji maamuzi ya upande mmoja
Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran adhuhuri ya jana Jumatatu aliwasili mjini New York akiuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Tehran kwa minajili ya kushiriki katika mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Akizungumza na waandishi wa habari alibainisha ratiba ya safari yake mjini New York. Rais wa…
Guterres: Afrika ni sehemu muhimu ya biashara na uwekezaji duniani
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Afrika ni sehemu muhimu ya biashara duniani na eneo kubwa la uwekezaji. Guterres ameyasema hayo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati wa uzinduzi wa mpango wa kimataifa wa kuimarisha biashara barani Afrika, Global African Business Initiative, GABI, wenye lengo la kuchagiza fursa za kibiashara…
Shirika la Kiislamu la ‘Who Is Hussain’ Uingereza lavunja rekodi ya dunia ya uchangiaji damu
Shirika moja la kutoa misaada la Kiislamu la Uingereza limevunja rekodi ya dunia kwa idadi kubwa zaidi ya uchangiaji damu katika mabara sita kwa siku moja pekee. Juhudi za rekodi ya dunia ziliongozwa mwezi Agosti na shirika la Kiislamu la kutoa misaada la haki za kijamii linalojulikana kama “Who Is Hussain,” ambalo lilikuwa linajaribu kuhamasisha…
Wafanyaziara milioni 1 na nusu watembelea Samarra Iraq baada ya Arubaini
Mji wa Samarra wenye haram mbili tukufu za Maimam wa Ahlul Bayt wa Bwana Mtume Muhammad SAW umeshuhudia wimbi kubwa la wafanyaziara waliolekea mjini humo baada ya kushiriki kwenye Arubaini ya Imam Husain AS huko Najaf na Karbala nchini Iraq. Taarifa kutoka nchini Iraq zinasema kuwa, zaidi ya wafanyaziara milioni 1 na laki tano wameelekea…
Uganda yakosoa EU kwa kupinga Bomba la Mafuta la Uganda -Tanzania
Wabunge nchini Uganda wamekosoa azimio la Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) lililosema nchi hiyo na Tanzania zinapaswa kusitisha miradi ya maendeleo ya mafuta na gesi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Wabunge wa EU walipitisha azimio hilo Alhamisi, wakitaja hatari kubwa za mazingira na hali ya hewa zinazosababishwa na Uganda, Tanzania na kampuni ya mafuta…
Aghalabu ya Wademocrat wanatilia shaka iwapo Biden atagombea urais 2024
Akthari ya wafuasi na wanachama wa chama cha Democrat nchini Marekani wametilia shaka uwezekano wa Rais Joe Biden wa nchi hiyo wa kugombea muhula wa pili katika uchaguzi ujao wa rais wa mwaka 2024. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na USA Today ikishirikiana na Ipsos unaonesha kuwa, asilimia 56 ya wapigakura wa chama cha Democratic hawaungi…
Bin Salman akaribishwa kwa maandamano nchini Uingereza
Makumi ya watetezi wa haki za binadamu wamefanya maandamano nje ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini London, kulaani safari ya Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman nchini Uingereza. Wananchi wa Uingereza pamoja na wakosoaji wa Saudia walioko London wameshiriki maandamano hayo ya kukosoa safari ya Bin Salman nchini humo, ambaye wanasema rekodi nyeusi…