
Iran inajitosheleza katika kuunda ndege zisizo na rubani (droni)
Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran inajitosheleza katika uundaji wa ndege zisizo na rubani (droni). Sekta ya ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hadi leo imekuwa na mafanikio mbalimbali nchini katika nyanja mbalimbali za nchi kavu, baharini, anga, na makombora. Aidha…

EFF: Hatumuombolezi Malkia Elizabeth kutokana na jinai za Uingereza
Chama cha The Economic Freedom Fighters (EFF) cha Afrika Kusini kimesema hakiombolezi kifo cha Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza aliyefariki jana. Taarifa ya EFF imesema Elizabeth alichukua hatamu za uongozi Uingereza mwaka 1952, na kutawala kwa miaka 70 kama mkuu wa ufalme ambao ulidumishwa na urithi wa kikatili wa kudhalilisha utu wa mamilioni ya…

Mazungumzo ya Maziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Afrika Kusini
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian amefanya mazungumzo ya simu na kubadilishana mawazo na Bi. Naledi Pandor, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, kuhusiana na masuala ya uhusiano pande mbili, kikanda na kimataifa. Akigusia umuhimu wa Bara la Afrika katika siasa za nje za Jamhuri ya…

Malkia Elizabeth II aliyetawala Uingereza kwa miaka 70 afariki
Malkia Elizabeth II wa Uingereza aliyeitawala nchi hiyo ya Ulaya kwa muda wa miaka 70 amefariki dunia Alhamisi akiwa na umri wamiaka 96 huku mustakabali wa ufalme anaouacha ukiwa matatani. Masaa machache kabla ya kifo chake, kasri ya Buckingham ilikuwa imetoa taarifa ikieleza wasiwasi juu ya afya ya Malkia huyo baada ya kufanyiwa tathmini ya afya…

Ugiriki yaonya juu ya kutokea vita vingine barani Ulaya sawa na vya Ukraine
Waziri wa mambo ya nje wa Ugiriki ametoa indhari ya kutokea vita vingine barani Ulaya kama vya Ukraine na kusisitiza kuwa iwapo Uturuki itaanzisha mashambulizi, Ugiriki itachukua hatua ya kujihami. Shirika la habari la Fars limeripoti leo kuwa, serikali ya Ugiriki imewaandikia barua washirika wake katika NATO, Umoja wa Ulaya na Katibu Mkuu wa…

Mazoezi ya vikosi vya nchi kavu vya jeshi; maonyesho ya nguvu na uwezo wa Iran ya Kiislamu
Mazoezi ya Uwezo 1401 ya jeshi la Iran yanafanyika kwa muda wa siku mbili kwa lengo la kutathmini na kuboresha kiwango cha nguvu na utayari wa kupambana wa Jkikosi cha Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na vitisho tarajiwa. Mazoezi hayo yalianza jana Jumatano kwa kushirikisha askari wa miguu, drone,…

Syria: Tutatumia haki yetu ya kisheria kujibu jinai za utawala haramu wa Israel
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imetangaza kuwa, mashambulio ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Uwanja wa Ndege wa Halab ni jinai za kivita na kwamba, Damascus itatumia haki yake ya kisheria kwa ajili ya kujibu jinai za utawala huo. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imeeleza kwamba, mashambulio…

Rais wa Lebanon: Hizbullah ni mshirika wetu na tunaiunga mkono
Rais Michel Aoun wa Lebanon amesisitiza kuwa anaiunga mkono Hizbullah na akabainisha kwamba, hatua iliyochukuliwa na muqawama wa Lebanon imesukuma mbele mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana ya kuainisha mipaka ya bahari. Mzozo kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Lebanon kuhusu mipaka ya bahari ya pande hizo mbili umeongezeka, huku Wazayuni wakiwa wanavikodolea…