Vyombo vya Habari

Israel yaua shahidi Wapalestina 2; yashambulia Syria kwa makombora

Israel yaua shahidi Wapalestina 2; yashambulia Syria kwa makombora

Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendeleza jinai na chokochoko zake dhidi ya mataifa mawili ya Waislamu katika eneo hili la Asia Magharibi. Wanajeshi makatili wa utawala huo pandikizi wamewaua shahidi mabarobaro wawili wa kiume wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kituo cha Habari cha Palestina kimeripoti kuwa, vijana hao wa Kipalestina Yazan Afana…

Kanada na Uingereza zilishirikiana kusafirisha wasichana kujiunga na magaidi wa Daesh

Kanada na Uingereza zilishirikiana kusafirisha wasichana kujiunga na magaidi wa Daesh

Idara ya ujasusi ya Kanada ilihusika katika kutuma wasichana kwenda kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh au ISIS na serikali ya Uingereza ilijua nafasi ya Kanada katika kashfaa hiyo lakini ikajizuia kuifichua. Hayo yamefichuliwa na mwandishi ambaye anaeleza kuhusu kisa cha Shamima Begum, raia wa zamani wa Uingereza ambaye alijiunga na ISIS mwaka 2015 akiwa na…

Russia: Mashambulizi dhidi ya Syria yamefichua undumakuwili wa Magharibi

Russia: Mashambulizi dhidi ya Syria yamefichua undumakuwili wa Magharibi

Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amelaani vikali mashambulio haramu ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria na kusisitiza kuwa, hujuma hizo zimefichua sura halisi ya Wamagharibi likija suala la haki za binadamu. Vasily Nebenzia amesema hayo katika hotuba yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa, “Israel…

Waziri Mkuu wa Iraq kujiuzulu iwapo mkwamo wa kisiasa utaendelea kushuhudiwa

Waziri Mkuu wa Iraq kujiuzulu iwapo mkwamo wa kisiasa utaendelea kushuhudiwa

Waziri Mkuu wa Iraq ametishia kuwa atajiuzulu wadhifa wake huo iwapo mkwamo na mgogoro wa kisiasa utaendelea kushuhudiwa nchini huo. Mustafa al-Kadhimi alitoa indhari hiyo jana Jumanne na kusisitiza kuwa, “Nitaachia ngazi kulalamikia hali ya kisiasa isiyoeleweka.” Taifa hilo la Kiarabu limekuwa katika mvutano wa kisiasa, uliopelekea kushindwa kuunda serikali tangu baada ya uchaguzi wa…

Waziri Mkuu wa Japan aahidi kufuatilia kiti cha Afrika katika Baraza la Usalama

Waziri Mkuu wa Japan aahidi kufuatilia kiti cha Afrika katika Baraza la Usalama

Waziri Mkuu wa Japan amesema kuwa, nchi yake ina mpango wa kustafidi na nafasi na ushawishi wake katika Baraza la Usalama ili kuhakikisha kuwa, bara la Afrika linapatiwa kiti cha kudumu katika taasisi hiyo muhimu duniani. Fumio Kishida, Waziri Mkuu wa Japan amesema hayo katika hotuba yake kwenye “Mkutano wa Kimataiifa wa Tokyo Kwa Ajili ya Ustawi…

Raisi: Kuimarishwa uhusiano wa Saudi Arabia na Iran ni kwa maslahi ya usalama wa eneo

Raisi: Kuimarishwa uhusiano wa Saudi Arabia na Iran ni kwa maslahi ya usalama wa eneo

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ubunifu na hatua za Iraq katika kuboresha ushirikiano baina ya nchi za eneo bila uingiliaji wa madola ajinabi ni jambo ambalo limekuwa na taathira na kuongeza kuwa: “Kurekebishwa na kuimarishwa uhusiano wa Iran na Saudi Arabia ni kwa maslahi ya usalama wa eneo.” Kwa mujibu wa taarifa,…

Russia: Marekani irejeshe fedha za Afghanistan zilizoibwa

Russia: Marekani irejeshe fedha za Afghanistan zilizoibwa

Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa ameitaka Marekani izirejeshe fedha zilizoibiwa Afghanistan. Vasily Nebenzya ametoa mwito huo alipohutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa shirika la habari la Russia TASS, mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kujadili suala la Afghanistan uligeuka uwanja wa utoaji tuhuma…

Wamarekani: Ndani ya miaka 10 ijayo vita vya wenyewe kwa wenyewe vitatokea nchini

Wamarekani: Ndani ya miaka 10 ijayo vita vya wenyewe kwa wenyewe vitatokea nchini

Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni yanaonyesha kuwa zaidi ya 40% ya Wamarekani wanaamini kwamba ndani ya miaka 10 ijayo, vita vya wenyewe kwa wenyewe vitatokea nchini humo. Kugunduliwa hati zaidi ya 300 zenye muhuri wa siri kwenye nyumba ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kumeshadidisha mvutano kati ya serikali ya Wademocrat na Trump…