
Takwimu mpya za kutisha zatolewa kuhusu jinai za Saudia nchini Yemen
Wizara ya Afya ya Yemen imetangaza takwimu mpya za hasara roho na mali za watu zilizosababishwa na jinai za miaka minane ya vita vya kivamizi vya muungano wa nchi za Kiarabu wakiongozwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati). Mwaka 2015, Saudia na Imarati kwa baraka kamili za Marekani, nchi za Magharibi…

Nusu ya wananchi wa Saudia wanalalamikia ugumu wa maisha
Uchunguzi wa hivi karibuni kabisa wa maoni unaonesha kuwa, nusu ya wananchi wa Saudia Arabia wanalalamikia ugumu wa maisha na kupanda vibaya kwa bei za bidhaa. Kwa mujibu wa al Khalij al Jadid, uchunguzi huo wa maoni umefanywa na shirika moja la kibiashara la eneo hili baada ya kuombwa kufanya hivyo na taasisi ya Marekani…

Azimio la Ukraine dhidi ya Russia katika Umoja wa Mataifa lapingwa na nchi nyingi
Rasimu ya azimio la Ukraine la kutaka Russia ilaaniwe katika Umoja wa Mataifa limegonga mwamba baada ya kupingwa na aghalabu ya nchi za dunia. Azimio hilo limeungwa mkono na nchi 58 pekee kati ya nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwa ni idadi ndogo sana ikilianganishwa na nchi ambazo ziliunga mkono Kiev mwezi…

Mashambulizi haramu ya Marekani nchini Syria, nembo ya ubeberu wa Washington
John Kriby, mratibu wa mahusiano ya kiistratijia ya baraza la usalama wa taifa la ikulu ya Marekani, White House amejaribu kuhalalalisha mashambulio haramu ya nchi yake huko Syria na kudai kuwa, eti Washington haina nia ya kuzidisha machafuko katika eneo hili. Vile vile amedai kuwa, lengo la mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani huko Syria…

Onyo la China kwa Canada kuhusu safari ya wabunge wake Taiwan
China imeionya vikali Canada na kusisitiza kuwa itachukua hatua madhubuti na za nguvu iwapo wabunge wa Canada watafanya safari ya kuitembelea Taiwan karibuni hivi. Taarifa ya Ubalozi wa China nchini Canada imesisitiza kuwa, safari tarajiwa ya Wabunge wa Canada katika eneo la Taiwan kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari wiki iliyopita, itakuwa na matokeo mabaya…

UN yataka dunia iwasaidie wakimbizi Waislamu wa Rohingya
Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuwasaidia kwa hali na mali wakimbizi Waislamu wa Rohingya walioko nchini Bangladesh. Noeleen Heyzer alitoa mwito huo Alkhamisi usiku katika siku ya nne ya safari yake ya kuitembelea Bangladesh na kusisitiza kuwa, Wabangladesh wameendelea kuwa wakarimu kwa wakimbizi Warohingya, na…

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran akutana na Rais wa Zanzibar
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu7 ya Iran aliyeko ziarani nchini Tanzania leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar na wawili hao wamesitizia udharura wa kuimarishwa ushirikiano baina ya pande mbili. Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar ameashiria katika mazungumzo yake na Hussein Amir-Abdollahian kuhusu uhusiano mkongwe baina ya…

Watu 180 waaga dunia kutokana na mafuriko nchini Afghanistan
Watu wasiopungua 180 wamefariki dunia nchini Afghanistan kutokana na mafuriko na matukio yanayohusiana na mvua kali zilizonyesha hivi karibuni. Msemaji wa serikali ya Taliban nchini humo, Zabihullah Mujahid amesema mbali na watu 182 kuaga dunia kwenye janga hilo la kimaumbile, wengine zaidi ya 250 wamejeruhiwa. Amesema nyumba zaidi ya 3,000 zimesombwa na maji ya mafuriko hayo na…