Serikali ya Chad imeitaka Ufaransa kuwa imewaondoa wanajeshi wake katika ardhi yake ifikapo Januari 31.
Imethibitishwa kwamba takwa hili liliwasilishwa huko Paris jana Disemba 19. Hata hivyo, afisa wa ngazi ya juu wa kijeshi wa Ufaransa, ameviambia vyombo vya habari, kwamba itakuwa vigumu kuondoa kikosi kizima cha jeshi katika kipindi cha wiki saba.
N’Djamena inasema ni bora kuondoka wanajeshi wa Ufaransa kabla ya mwisho wa mwezi Februari na kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mwishoni mwa mwezi uliopita wa Novemba, Chad ilihitimisha makubaliano yake ya kijeshi na Ufaransa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika nyanja za usalama na ulinzi kati ya nchi mbili.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Chad ilieleza kuwa serikali ya Jamhuri ya Chad inaeleza maoni ya kitaifa na kimataifa kuhusu uamuzi wake wa kusitisha mkataba wa ushirikiano wa kiulinzi uliousaini na Ufaransa.
Taarifa ilisainiwa na Abderaman Koulamallah, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad ilieleza kuwa baada ya miongo kadhaa ya uhuru wa nchi wakati umefika sasa kwa Chad kuwa na mamlaka kamili na kutazama upya ushirikiano wake wa kimkakati kwa mujibu wa maslahi ya taifa.”