Chuo kikuu cha Daystar Kenya chafuta mkataba na ‘Israel’ baada ya malalamiko ya umma

Siku mbili tu baada ya Chuo Kikuu cha Daystar cha Kenya kutia saini mkataba na ubalozi wa utawala Israel  jijini Nairobi  kuanzisha ‘Msitu wa Zion’ kwenye chuo chake, taasisi hiyo imebatilisha uamuzi wake kufuatia hasira za wananchi katika mitandao ya kijamii hasa X.

Makubaliano hayo, yaliyotangazwa Jumatatu, yalilenga kupanda miti 5,000 ‘ya kibiblia’ kwenye uwanja wa chuo kikuu hichi lakini punde baada ya habari za mkataba huo kusamabaa, Wakenya, wakiwemo wanafunzi wa zamani wa chuo hicho, waliupinga vikali kutokana na mauaji ya kimbari yanayoendelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza..

Kampeni ilizinduliwa haraka mitandaoni ikitaka mkataba huo ubatilishwe huku wengi wakishutumu chuo hicho kwa kuunga mkono jinai za  Israel huko Palestina.

David Ngira, mtumiaji wa mtanadao wa kijamii wa X, alielezea kusikitishwa kwake, akisema, “Ni aibu kwa Chuo Kikuu cha Daystar kutia saini mkataba na utawala wa ubaguzi wa rangi ambao unafanya mauaji ya kimbari.” Amesema wanapinga  mkataba huo hasa kutokana na historia ya Kenya kupiga vita ukoloni na ubaguzi wa rangi.

Mohammed Husny alitumia akaunti yake ya X kulaani hatua hiyo, akisema, “Ni aibu kwamba chuo kikuu kitaingia kitandani na utawala wa Kizayuni  wakati utawala huu umeshambulia kwa mabomu kila taasisi ya elimu huko Gaza na kuwaua kwa makusudi wasomi huko Palestina ili kuzuia taarifa  sahihi za mauaji yao ya kimbari.”

Naye mtumiaji mwingine wa mitandao ya kijamii, Araget amesema, “Chuo Kikuu cha Daystar kinaonyesha kuunga mkono utawala wa Kizayuni wenye kutekeleza mauaji ya kimbari Inatisha.”

Mtumiaji mwingine wa X anayejulikana kama Emmy alihoji, “Kituo cha elimu kinaungana na utawala ambao umekuwa ukifanya mauaji ya kimbari i na kuzishambulia kwa mabomu taasisi za elimu nchini Palestina, je, kuna kuzama chini kabisa zaidi ya huku?”

Wathanga Gatimu ameandika kwenye X kwamba: “Israel ndie mhusika mkuu wa ugaidi duniani. Serikali yetu haiwakilishi hisia za Wakenya walio wengi. Tunasimama na haki ya Palestina ya mapambano dhidi utawala wa Israel, amba oni utawala wa wauaji wa watoto na wabakaji.”

Kufuatia malamiko ya Wakenya Kansela  wa chuo hicho Profesa Laban Ayiro alitangaza kubatilisha mkataba huo akisisitiza kuwa taasisi hiyo haiungi jinai dhidi ya kibinadamu zinazoendelea ‘Mashariki ya Kati.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *