Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN) chapuuza shahada ya Naibu Rais ‘William Kipchirchir Ruto’ ambayo imeenea mitandaoni

Kwa sasa mgombea huyo ana digrii tatu kutoka kwenye taasisi hiyo.

Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN) kimejitokeza kufafanua kuwa waraka unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kua ni shahada ya digrii aliyokabidhiwa naibu Rais nchini Kenya Bw. William Ruto ni ghushi.

Ukweli ni kwamba naibu rais alijiandikisha kwa Shahada ya Kwanza baada ya kukamilisha masomo yake ya ngazi ya kwanza ‘A-Level’ katika Shule ya Upili ya Kapsabet iliyomokwenye Kaunti ya Nandi. Alijihusisha na elimu ya Zoolojia na Botania kabla ya kuhitimu mwaka wa 1990.

Mara tu baada ya kuhitimu masomo yake, mwanasiasa huyo mzoefu alipewa ufadhili wa kusomea Shahada ya Uzamili katika taasisi hiyo lakini ikabidi aahirishe masomo yake ili kujishughulisha na mambo mengine.

Mwaka wa 2008, akiwa Waziri wa Kilimo, alihitimu Shahada ya Uzamili ya Ikolojia ya Mimea.

Muongo mmoja baadaye, mnamo Desemba 2018, Naibu Rais Ruto alikuwa miongoni mwa wahitimu katika taasisi hiyo hiyo na kupata PhD katika Ikolojia ya Mimea.

Matukio hayo yamejiri baada ya kuibuka kuwa Seneta Sakaja hakuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi alikokuwa kiongozi wa wanafunzi.

Malalamiko manne tayari yamewasilishwa ya kutaka Sakaja asishiriki katika Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *