CNN: Saudia inaelekea kuwa kitovu cha matumizi ya madawa ya kulevya Mashariki ya Kati

Televisheni ya CNN ya Marekani imetangaza habari ya kukamatwa kete karibu milioni 47 za madawa ya kulevya nchini Saudi Arabia na kuongeza kuwa, nchi hiyo ya kifalme hivi sasa inaelekea kuwa kitovu cha matumizi ya mihadarati katika eneo la Mashariki ya Kati.

Katika taarifa yake hiyo, televisheni ya CNN ya Marekani imetangaza kwamba, siku ya Jumatano, maafisa wa Saudi Arabia walikamata shehena kubwa sana ya madawa ya kulevya mjini Riyadh, hatua ambayo imezidi kuthibitisha maneno ya wataalamu wa mambo kuwa kiwango cha matumizi ya madawa ya kulevya kimeongezeka sana nchini Saudia hivi sasa na inaelekea kuwa kitovu cha matumizi ya madawa hayo haramu katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa muda sasa vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimekuwa vikilalamikia ongezeko la madawa ya kulevya nchini humo huku mwandishi mmoja akisema kuwa, kukamatwa shehena hiyo kubwa ya mihadarati kunaonesha kuweko vita maalumu dhidi ya taifa hilo la Kiarabu. Mwandishi huyo alisema, vita vya kuingizwa mihadarati nchini Saudi Arabia ni vikali na vikubwa zaidi kuliko vita vingine vyovyote.

Siku ya Jumatano, maafisa wa Saudia walitangaza kukamatwa shehena kubwa zaidi ya madawa ya kulevya, yaani karibu vidonge milioni 47 vya madawa hayo haramu ambavyo vilikuwa vimefichwa kwenye shehena nne tofauti huko Riyadh.

Televisheni ya CNN imeongeza kuwa, madawa mengi ya kulevya yanayokamatwa katika nchi za Mashariki ya Kati huwa na logo ya Captagon. Kiasili Captagon ni nembo ya utengenezaji na uzalishaji madawa yaliyokuwa na athari za kulevya na hivi sasa nembo hiyo imepigwa marufuku kuzalisha madawa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *