Rais wa Brazil ametangaza kuwa nchi yake itawaunga mkono na kuwatetea kwa dhati Wapalestina.
Rais wa Brazil Luis Inacio Lula da Silva ameyasema hayo katika kikao chake na Riyad al-Maliki, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ambaye alimwakilisha Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas katika sherehe za kuapishwa kwake, na kusisitiza kwa mara nyingine azma ya nchi yake ya kuunga mkono harakati za ukombozi za taifa la Palestina.
Da Silva ameongeza kuwa Brazil itajitahidi kurejesha uhuru wa Palestina kama nchi huru na inayojitawala ndani ya mipaka ya 1967.
Rais wa Jamhuri ya Brazil amesema kuwa Brasilia itaunga mkono juhudi za Palestina katika nyanja zote za kimataifa na kuashiria kuwa nchi yake itaendelea kuwa msaidizi wa Palestina.
Luiz Inacio Lula da Silva, anayejulikana kama “Lula”, aliapishwa kama Rais wa Brazil kwa mara ya tatu Jumapili iliyopita.
Wataalamu wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa Da Silva atakuwa na jukumu la kusaidia Palestina katika kipindi cha sasa; suala ambalo limeutia wahka na wasiwasi mkubwa utawala wa Kizayuni wa Israel.