Daktari Muirani atunukiwa tuzo ya juu ya kielimu ya daktari bingwa wa mfumo wa mkojo duniani

Profesa Nasser Simforoosh wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Shahid Beheshti cha Iran ameshinda tuzo ya kielimu ya juu ambayo hutolewa kwa madaktari bora duniani katika fani ya mfumo wa mkojo (Urorogist).

Dakta Simforoosh ambaye ni mhadhiri na mwanachama wa Akademia ya Kisayansi katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Shahid Beheshti cha hapa Iran atapokea tuzo hiyo ya juu ya kielimu kwa jina la SIU (Distinguished Career Award) katika Kongamano la Kimataifa la Masuala ya Tiba ya Mfumo wa Mkojo huko Montreal nchini Canada.  Madaktari bingwa zaidi ya elfu tano wa tiba ya mfumo wa mkojo duniani watashiriki katika kongamano hilo huko Canada.

Tuzo hiyo ya SIU ni moja ya tuzo kubwa na muhimu zaidi iliyo na itibari ya juu ya kielimu kimataifa; na hutolewa kwa shakhsia ambao wamekuwa na taathira na kufanya kazi kubwa ya kitiba katika masuala ya maradhi ya mfumo wa mkojo.

Kutunukiwa tuzo hii sio mafanikio ya wakati mmoja tu  bali ni  mafanikio ya kitaaluma ya maisha yote yanayopatikana katika kipindi cha utoaji huduma kama daktari mbobezi wa masuala ya mfumo wa mkojo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *